Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 8:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari bili, ukashikamane nalo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda karibu na gari hilo ukafuatane nalo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda karibu na gari hilo ukafuatane nalo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda karibu na gari hilo ukafuatane nalo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Roho wa Mungu akamwambia Filipo, “Nenda kwenye lile gari ukae karibu nalo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Roho wa Mwenyezi Mungu akamwambia Filipo, “Nenda kwenye lile gari ukae karibu nalo.”

Tazama sura Nakili




Matendo 8:29
16 Marejeleo ya Msalaba  

Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutaka.


Roho akaniambia nifuatane nao, nisione mashaka. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule:


Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paolo akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemi watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa mataifa.


Na walipokuwa hawapatani wao kwawao, wakaenda zao, Paolo alipokwisha kusema neno hili moja ya kama, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,


Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka uende upande wa kusini hatta njia ile itelemkayo kutoka Yemsalemi kwenda Gaza; nayo ni jangwa.


nae amekwenda Yerusalemi kuabudu, akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya.


Bassi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya: akanena, Je, yamekuelea haya unayosoma?


Kiisha, walipotoka majini, Roho ya Bwana ikamnyakua Filipo, yule tawashi asimwone tena; maana alikwenda zake akifurahi:


lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yule yule, akimgawia killa mmoja peke yake kama apendavyo yeye.


ROHO yanena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho watu watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani,


Kwa hiyo, kama anenavyo Robo Mtakatifu, Leo, kama mtasikia sauti yake,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo