Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 6:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Neno hili likapendeza machoni jia mkutano wote: wakamehagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu na Filipo, na Prokoro, na Nikanor, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Jambo hilo likaipendeza jumuiya yote ya waumini. Wakawachagua Stefano, mtu mwenye imani kubwa na mwenye kujaa Roho Mtakatifu, Filipo, Prokoro, Nikanori, Timona, Parmena na Nikolao wa Antiokia ambaye wakati mmoja alikuwa ameongokea dini ya Kiyahudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Jambo hilo likaipendeza jumuiya yote ya waumini. Wakawachagua Stefano, mtu mwenye imani kubwa na mwenye kujaa Roho Mtakatifu, Filipo, Prokoro, Nikanori, Timona, Parmena na Nikolao wa Antiokia ambaye wakati mmoja alikuwa ameongokea dini ya Kiyahudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Jambo hilo likaipendeza jumuiya yote ya waumini. Wakawachagua Stefano, mtu mwenye imani kubwa na mwenye kujaa Roho Mtakatifu, Filipo, Prokoro, Nikanori, Timona, Parmena na Nikolao wa Antiokia ambaye wakati mmoja alikuwa ameongokea dini ya Kiyahudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Yale waliyosema yakawapendeza watu wote, nao wakamchagua Stefano (mtu aliyejawa na imani na Roho wa Mungu) pamoja na Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena na Nikolao kutoka Antiokia, mtu wa Mataifa aliyeongokea dini ya Kiyahudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Yale waliyosema yakawapendeza watu wote, nao wakamchagua Stefano (mtu aliyejawa na imani na Roho wa Mwenyezi Mungu) pamoja na Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena na Nikolao, mwongofu kutoka Antiokia.

Tazama sura Nakili




Matendo 6:5
24 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnazunguka katika bahari na inchi kavu illi kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehannum marra mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.


Bassi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shidda iliyotukia kwa khabari ya Stefano, wakasafiri hatta Foiniki na Kupro na Antiokia, wasilikhubiri lile neno illa kwa Wayahudi peke yao.


Baadhi ya hao walikuwa watu wa Kupro na Kurene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wahelenisti, wakakhubiri khabari njema za Bwana Yesu.


Khabari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wakaintuma Barnaba, aende hatta Antiokia.


Maana alikuwa mtu mwema, amejaa Roho Mtakatifu na imani: watu wengi wakajitia upande wa Bwana.


Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hajio Antiokia.


Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yemsalemi hatta Antiokia.


NA huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, Barnaba na Sumeon aitwae Niger, na Lukio Mkurene, na Manaen aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Herode mfalme, na Saul.


Bassi ikawapendeza mitume na wazee na Kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paolo na Barnaba: nao ni hawa, Yuda aliyekwitwa Barsaba, na Sila, watu wakuu katika ndugu.


Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha mbalimbali, kama Roho alivyowajalia kutamka.


Assubuhi yake sisi tulifuatana na Paolo tukatoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, Mwinjilisti, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.


Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali auawe, nikizitunza nguo zao waliomwua.


lakini hawakuweza kushindana na hekima yake wala na Roho aliyosema nayo.


Bassi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, illi tuwaweke juu ya jambo hili:


Na Stefano, akijaa imani na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.


KUHANI mkuu akasema, Je! Mambo hayo ndivyo yalivyo?


Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolaiti, niyachukiayo.


Lakmi unalo neno hili kwamba wayachukia matendo ya Wanikolaiti, niyachukiayo na mimi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo