Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 6:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA siku ziie wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manungʼuniko ya Wahelenisti juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika khuduma ya killa siku.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manunguniko kati ya waumini walioongea Kigiriki na wale walioongea Kiebrania. Wale walioongea Kigiriki walinungunika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manunguniko kati ya waumini walioongea Kigiriki na wale walioongea Kiebrania. Wale walioongea Kigiriki walinungunika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Baadaye, idadi ya wanafunzi ilipokuwa inazidi kuongezeka, kulitokea manung'uniko kati ya waumini walioongea Kigiriki na wale walioongea Kiebrania. Wale walioongea Kigiriki walinung'unika kwamba wajane wao walikuwa wanasahauliwa katika ugawaji wa mahitaji ya kila siku.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, Wayahudi wa Kiyunani walinung’unika dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawo wa chakula wa kila siku.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Basi ikawa katika siku hizo, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa ikiongezeka sana, palitokea manung’uniko kati ya Wayahudi wa Kiyunani, dhidi ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahaulika katika mgawanyo wa chakula wa kila siku.

Tazama sura Nakili




Matendo 6:1
38 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.


Baadhi ya hao walikuwa watu wa Kupro na Kurene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wahelenisti, wakakhubiri khabari njema za Bwana Yesu.


Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hajio Antiokia.


Na wale wanafunzi, killa mtu kwa kadiri alivyofanikiwa wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Yahudi.


Nao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa: na siku ile wakazidishiwa watu wapata elfu tatu.


wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama killa mtu alivyokuwa na haja.


wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.


wakaiweka miguuni jia mitume; killa mtu akagawiwa kwa kadiri alivyohitaji.


Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini: na hesabu ya watu ilikuwa kama elfu tano.


waamini wakazidi kuja kwa Bwana, wengi, wanaume ha wanawake:


Je! hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili: nanyi mmeijaza Yerusalemi mafundisho yenu, na mnataka kuleta damu ya mtu yule juu yetu.


Wale thenashara wakawaita jamii va wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kukhudumu mezani.


Nenu la Mungu likaenea: hesahu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemi: jamii kubwa la makuhani wakaitii Imani.


Akaneua kwa jina lake Yesu pasipo khofu, akinena na kushindana na Wahelenisti. Nao wakajaribu kumwua.


Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika wakampeleka juu orofani: wajane wote wakasimama karibu nae, wakilia na kuniwonyesha zile kanzu na nguo alizozifanya Paa wakati ule alipokuwa pamoja nao.


Akampa mkono, akamwinua; hatta akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, yu hayi.


ikiwa khuduma, tuwemo katika khuduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;


Wala msinungʼunike, kama wengine wao walivyommgʼunika, wakaharibiwa na mharabu.


Wao Waebrania? Na mimi. Wao Waisraeli? Na mimi. Wao uzao wa Ibrahimu? Na mimi.


Nalitabiriwa siku ya nane, ni lutu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benjamin, Mwebrania wa Waebrania, kwa khabari ya kuifuata sharia, Farisayo, kwa khabari ya wivu, mwenye kuliudhi Kanisa,


Waheshimu wajane walio wajane kweli kweli.


Mjane aandikwe, ikiwa umri wake amepata miaka sittini, isipungue, nae amekuwa mke wa mume mmoja,


Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.


Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema burre? Roho ikaayo ndani yetu hutamani kiasi cha kuona wivu?


Msinungʼunikiane, ndugu, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo