Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 5:42 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

42 Na killa siku ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kukhubiri khabari njema za Yesu kwamba ni Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Wakaendelea kila siku kufundisha na kuhubiri Habari Njema ya Kristo hekaluni na nyumbani kwa watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 Wakaendelea kila siku kufundisha na kuhubiri Habari Njema ya Kristo hekaluni na nyumbani kwa watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Wakaendelea kila siku kufundisha na kuhubiri Habari Njema ya Kristo hekaluni na nyumbani kwa watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri Habari Njema kwamba Isa ndiye Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema kwamba Isa ndiye Al-Masihi.

Tazama sura Nakili




Matendo 5:42
22 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi killa siku alikuwa akifundisha hekaluni wakati wa mchana; na wakati wa usiku akitoka, na kulala katika mlima uitwao mlima wa mizeituni.


Killa siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono; lakini saa yenu hii, na mamlaka ya giza.


Baadhi ya hao walikuwa watu wa Kupro na Kurene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wahelenisti, wakakhubiri khabari njema za Bwana Yesu.


Na sisi tunawakhubirieni ahadi ile waliyopewa baba zetu, ya kwamba Mungu ametutimizia sisi watoto wao ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu:


Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo.


akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kama, Yesu huyu ninaewapasha ninyi khabari zake ndiye Kristo.


Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kupokea chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe,


ya kuwa sikuficha neno lo lote liwezaio kuwafaeni, bali naliwaonyesha na kuwafundisha kwa wazi na nyumba kwa nyumba,


Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.


Bassi sasa, Bwana, yaangalie maogofya yao; ukawajalie watumishi wako kunena neno lako kwa uthabiti,


Filipo akafunua kinywa chake na akilianzia andiko hili, akamkhubiri khabari njema za Yesu.


Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawakhubiri Kristo.


Marra akamkhubiri Yesu katika masunagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.


Maana naliazimu nisijue neno kwenu illa Yesu Kristo, nae amesulibiwa.


alipoona vema kumdhihirisha Mwana wake ndani yangu, illi niwakhubiri mataifa khabari zake, marra sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu,


Lakini mimi, hasha nisijisifie kitu illa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo