Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 5:40 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

40 Wakakubali maneno yake; wakawaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kiisha wakawaacha waende zao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 Hivyo wakawaita wale mitume, wakaamuru wachapwe viboko na kuwaonya wasifundishe tena kwa jina la Yesu; kisha wakawaacha waende zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

40 Hivyo wakawaita wale mitume, wakaamuru wachapwe viboko na kuwaonya wasifundishe tena kwa jina la Yesu; kisha wakawaacha waende zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 Hivyo wakawaita wale mitume, wakaamuru wachapwe viboko na kuwaonya wasifundishe tena kwa jina la Yesu; kisha wakawaacha waende zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 Wakapokea ushauri wa Gamalieli. Wakawaita mitume ndani, wakaamuru wachapwe mijeledi, kisha wakawaagiza wasinene tena kwa jina la Isa, wakawaachia waende zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 Wakapokea ushauri wa Gamalieli. Wakawaita mitume ndani, wakaamuru wachapwe mijeledi, kisha wakawaagiza wasinene tena kwa jina la Isa, wakawaachia waende zao.

Tazama sura Nakili

Matendo 5:40
13 Marejeleo ya Msalaba  

Jihadharini na wana Adamu; kwa maana watawapelekeni mbele ya baraza, na katika masunagogi yao watawapiga;

na watampeleka kwa Mataifa wapate kumdhihaki, na kumpiga mijeledi, na kumsulibi; na siku ya tatu atafufuka.

Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji;

Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.

Na wakati wa mavuno akatuma mtumishi kwa wale wakulima illi wampe baadhi ya matunda ya mizabibu, wakulima wakampiga, wakamtoa hana kitu.

Je! hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili: nanyi mmeijaza Yerusalemi mafundisho yenu, na mnataka kuleta damu ya mtu yule juu yetu.

Kwa Wayahudi marra tano nalipata mapigo arubaini kasoro moja.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo