Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 5:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamaliel, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Lakini Mfarisayo mmoja aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa sheria na aliyeheshimika sana mbele ya watu wote, alisimama mbele ya lile Baraza, akataka wale mitume watolewe nje kwa muda mfupi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Lakini Mfarisayo mmoja aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa sheria na aliyeheshimika sana mbele ya watu wote, alisimama mbele ya lile Baraza, akataka wale mitume watolewe nje kwa muda mfupi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Lakini Mfarisayo mmoja aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa sheria na aliyeheshimika sana mbele ya watu wote, alisimama mbele ya lile Baraza, akataka wale mitume watolewe nje kwa muda mfupi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Lakini Farisayo mmoja, jina lake Gamalieli, aliyekuwa mwalimu wa Torati, aliyeheshimiwa na watu wote, akasimama mbele ya Baraza la Wayahudi, akaamuru mitume watolewe nje kwa muda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Lakini Farisayo mmoja, jina lake Gamalieli, aliyekuwa mwalimu wa Torati, aliyeheshimiwa na watu wote, akasimama mbele ya baraza akaamuru mitume watolewe nje kwa muda.

Tazama sura Nakili




Matendo 5:34
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa baada ya siku tatu, wakamwona hekaluni, ameketi kati ya waalimu, akiwasikiliza, na kuwauliza.


Hatta siku moja ya siku zile alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waandishi wameketi, waliokuwa wametoka katika killa kijiji cha Galilaya, na cha Yahudi, na Yerusalemi; uweza wa Bwana ulikuwa pamoja nae apate kuwaponya.


Yesu akajibu akamwambia, Je! Wewe u mwalimu katika Israeli, na haya huyafahamu?


Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, nikalelewa katika niji huu miguumi pa Gamaliel, nikafundishwa sharia ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa ijtihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi:


Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakafanya shauri, wakisemii, Tuwafanyieni watu hawa?


Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja kuhani mkuu nao walio pamoja nae, wakawaita watu wa haraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani illi wawalete.


Wakawaleta, wakaweka katika baraza. Kuhani mkuu akawauliza, akisema,


akaamuru mitume wawekwe nje kitambo, akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda watu hawa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo