Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 5:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Nao waliposikia wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja kuhani mkuu nao walio pamoja nae, wakawaita watu wa haraza, na wazee wote wa wana wa Israeli, wakatuma watu gerezani illi wawalete.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Mitume walitii, wakaingia hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza kufundisha. Kuhani mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu na halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi, halafu wakawatuma watu gerezani wawalete wale mitume.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Mitume walitii, wakaingia hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza kufundisha. Kuhani mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu na halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi, halafu wakawatuma watu gerezani wawalete wale mitume.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Mitume walitii, wakaingia hekaluni asubuhi na mapema, wakaanza kufundisha. Kuhani mkuu na wenzake walipofika, waliita mkutano wa Baraza kuu na halmashauri yote ya wazee wa Wayahudi, halafu wakawatuma watu gerezani wawalete wale mitume.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu. Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya Baraza la Wayahudi, yaani wazee wote wa Israeli. Wakatumana wale mitume waletwe kutoka gerezani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu. Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani.

Tazama sura Nakili

Matendo 5:21
16 Marejeleo ya Msalaba  

Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.

Hatta ulipokuwa mchana wakakusanyika jamii ya wazee wa watu, na makuhani wakuu, na waandishi, wakamleta kwa haraza yao, wakisema,

Pilato akajibu, Je! mimi Myahudi? Taifa lako na makuhani wakuu ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?

Hatta assubuhi ilipokucha akaingia tena hekaluni, watu wote wakamwendea: nae akaketi akawa akiwafundisha.

Kwa maana utakuwa shahidi wake kwa watu wote, wa mambo hayo uliyoyaona na kuyasikia.

Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.

Akaondoka kuhani mkuu na wote waliokuwa pamoja nae (hao ndio walio wa madhehehu ya Masadukayo) wamejaa wivu,

Wakawaleta, wakaweka katika baraza. Kuhani mkuu akawauliza, akisema,

Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamaliel, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza,

Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya jina lake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo