Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 4:36 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

36 Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Kulikuwa na Mlawi mmoja, mzaliwa wa Kupro, jina lake Yosefu, ambaye mitume walimwita Barnaba (maana yake, “Mtu mwenye kutia moyo”).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Kulikuwa na Mlawi mmoja, mzaliwa wa Kupro, jina lake Yosefu, ambaye mitume walimwita Barnaba (maana yake, “Mtu mwenye kutia moyo”).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Kulikuwa na Mlawi mmoja, mzaliwa wa Kupro, jina lake Yosefu, ambaye mitume walimwita Barnaba (maana yake, “Mtu mwenye kutia moyo”).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Yusufu, Mlawi kutoka Kipro, ambaye mitume walimwita Barnaba (maana yake Mwana wa Faraja),

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 Yusufu, Mlawi kutoka Kipro, ambaye mitume walimwita Barnaba (maana yake Mwana wa Faraja),

Tazama sura Nakili




Matendo 4:36
24 Marejeleo ya Msalaba  

na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, akawapa jina, Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo,


Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaha na Saul.


Na Barnaba na Saul, walipokwisha kuitimiza khuduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemi wakamchukua pamoja nao Yohana aitwae Marko.


NA huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, Barnaba na Sumeon aitwae Niger, na Lukio Mkurene, na Manaen aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Herode mfalme, na Saul.


Kiisha baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sunagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni.


Bassi hawa walipokuwa wakimkhudumia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Niwekeeni Barnaba na Saul kwa kazi ile niliyowaitia.


Bassi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Selukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hatta Kupro.


Bassi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paolo wakiwapasha khabari za ishara na maajabu ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika mataifa.


Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo.


Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyekwitwa Marko pamoja nao.


Bassi palitokea maneno makali beina yao hatta wakatengana: Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kupro.


Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakachukua na Mnason, mtu wa Kupro, mwanafunzi wa zamani ambae ndiye tutakaekaa kwake.


Na tulipoona Kupro tukaiacha upande wa kushoto: tukasafiri hatta Shami tukashuka Turo. Kwa maana huko ndiko marikebu yetu itakakoshusha shehena yake.


Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kupro illi kuukinga upepo, kwa maana pepo zilikuwa za mbisho,


Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema nae, na jinsi alivyokhubiri pasipo khofu katika Dameski kwa jina lake Yesu.


Bali yeye akhutubuye, anena na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.


Au je! ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo kutokufanya kazi?


KIISHA, baada va miaka kumi na minane, nalipanda kwenda Yerusalemi pamoja na Barnaba, nikamchukua na Tito pamoja nami.


Na Wayahudi wakajigeuza pamoja nae, hatta Barnaba nae akachukuliwa na unafiki wao.


tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


Aristarko, aliyefumgwa pamoja nami, awasalimu, na Marko, mjomba wake Barnaba, amhae mmepokea maagizo kwa khabari yake; akifika kwenu mkaribisheni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo