Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 4:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na uwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Hakuna mtu yeyote aliyetindikiwa kitu, maana waliokuwa na mashamba au nyumba walikuwa wanaviuza

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Hakuna mtu yeyote aliyetindikiwa kitu, maana waliokuwa na mashamba au nyumba walikuwa wanaviuza

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Hakuna mtu yeyote aliyetindikiwa kitu, maana waliokuwa na mashamba au nyumba walikuwa wanaviuza

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Wala hapakuwa mtu yeyote miongoni mwao aliyekuwa mhitaji, kwa sababu mara kwa mara wale waliokuwa na mashamba na nyumba waliviuza, wakaleta thamani ya vitu vilivyouzwa,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Wala hapakuwepo mtu yeyote miongoni mwao aliyekuwa mhitaji, kwa sababu mara kwa mara wale waliokuwa na mashamba na nyumba waliviuza, wakaleta thamani ya vitu vilivyouzwa,

Tazama sura Nakili




Matendo 4:34
14 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate.


Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate.


Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.


Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele.


Akawaambia, Nilipowatuma bila mifuko na mkoba na viatu, mlipunguka kitu? Wakasema, Hapana.


wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama killa mtu alivyokuwa na haja.


alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.


bali mambo yawe sawa sawa: wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, illi na wingi wao uwafae ninyi upungufu wenu; illi mambo yawe sawa sawa.


illi mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na baja ya cho chote.


wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele.


Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo