Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 4:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Na jamii ya watu walioamini walikuwa moyo mmoja na roho moja: wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Jumuiya yote ya waumini ilikuwa na moyo mmoja na roho moja. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na kitu chochote akakiweka kuwa mali yake binafsi, ila waligawana vyote walivyokuwa navyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Jumuiya yote ya waumini ilikuwa na moyo mmoja na roho moja. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na kitu chochote akakiweka kuwa mali yake binafsi, ila waligawana vyote walivyokuwa navyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Jumuiya yote ya waumini ilikuwa na moyo mmoja na roho moja. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na kitu chochote akakiweka kuwa mali yake binafsi, ila waligawana vyote walivyokuwa navyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Waumini wote walikuwa na moyo mmoja na nia moja. Wala hakuna hata mmoja aliyesema chochote alichokuwa nacho ni mali yake mwenyewe, lakini walishirikiana kila kitu walichokuwa nacho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Wale walioamini wote walikuwa na moyo mmoja na nia moja. Wala hakuna hata mmoja aliyesema chochote alichokuwa nacho ni mali yake mwenyewe, lakini walishirikiana kila kitu walichokuwa nacho.

Tazama sura Nakili




Matendo 4:32
21 Marejeleo ya Msalaba  

Na mimi simo tena ulimwenguni, na hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, uwalinde kwa jina lako wale ulionipa; wawe moja, kama sisi.


Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kuomba, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama wake Yesu, na ndugu zake.


HATTA ilipotimia siku ya Pentekote walikuwako wote pamoja mahali pamoja.


Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu: nao wote walikuwa kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani:


vivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na sisi sote tu viungo killa mmoja kwa wenzake.


Nawasihi ninyi, ndugu, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mnene nyote mamoja, pasiwe kwenu faraka, bali mwe mmekhitimu katika nia moja na shauri moja.


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;


Neno la mwisbo ni hili; mwe na nia moja, wahurumianao, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo