Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 4:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Bassi sasa, Bwana, yaangalie maogofya yao; ukawajalie watumishi wako kunena neno lako kwa uthabiti,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Lakini sasa, ee Bwana, angalia vitisho vyao. Utuwezeshe sisi watumishi wako kuhubiri neno lako kwa uhodari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Lakini sasa, ee Bwana, angalia vitisho vyao. Utuwezeshe sisi watumishi wako kuhubiri neno lako kwa uhodari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Lakini sasa, ee Bwana, angalia vitisho vyao. Utuwezeshe sisi watumishi wako kuhubiri neno lako kwa uhodari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Sasa, Mwenyezi Mungu, angalia vitisho vyao na utuwezeshe sisi watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri mkuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Sasa, Bwana Mwenyezi, angalia vitisho vyao na utuwezeshe sisi watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri mkuu.

Tazama sura Nakili




Matendo 4:29
27 Marejeleo ya Msalaba  

Paolo na Barnaba wakanena kwa uthabiti wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza: illakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, wala hamjioni nafsi zenu kuwa mmestahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia mataifa.


Bassi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa uthabiti katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao.


Akaingia ndani ya sunagogi, akanena kwa ujasiri, akihujiana na watu kwa muda wa miezi mitatu, na kuwavuta waamini mambo ya ufalme wa Mungu.


Kwa maana mfalme anajua khabari za mambo haya, na naweza kusema nae bila khofu, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua; kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni.


Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.


Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka:


Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.


Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema nae, na jinsi alivyokhubiri pasipo khofu katika Dameski kwa jina lake Yesu.


Nae akawa pamoja nao katika Yerusalemi akiingia na kutoka.


Kwa hiyo yeye anenae kwa lugha na aombe apewe kufasiri.


Bassi, kwa kuwa tuna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi;


Na walio wengi wa ndugu walio katika Bwana, wakipata kuthubutika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kulinena neno la Bwana pasipo khofu.


bali tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filippi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.


Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, illi kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, mataifa wrote wakasikie; nikaokolewa katika kanwa la simba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo