Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 4:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Basi, hao wazee wa Baraza wakawaonya kwa ukali zaidi, halafu wakawaacha huru. Hawakuweza kuwapa adhabu kwa sababu watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa sababu ya tukio hilo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Basi, hao wazee wa Baraza wakawaonya kwa ukali zaidi, halafu wakawaacha huru. Hawakuweza kuwapa adhabu kwa sababu watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa sababu ya tukio hilo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Basi, hao wazee wa Baraza wakawaonya kwa ukali zaidi, halafu wakawaacha huru. Hawakuweza kuwapa adhabu kwa sababu watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa sababu ya tukio hilo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Baada ya vitisho vingi, wakawaachia waende zao. Hawakuona njia yoyote ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu, kwa kuwa watu wote walikuwa wakimsifu Mungu kwa kile kilichokuwa kimetukia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Baada ya vitisho vingi, wakawaacha waende zao. Hawakuona njia yoyote ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu, kwa kuwa watu wote walikuwa wakimsifu Mungu kwa kile kilichokuwa kimetukia.

Tazama sura Nakili




Matendo 4:21
18 Marejeleo ya Msalaba  

hatta makutano wakastaajabu, walipowaona bubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.


Nao walipotafuta kumkamata, wakawaogopa makutano, kwa maana walimwona kuwa nabii.


Wakanena, Sio wakati wa siku kuu, isije ikatokea ghasia katika watu.


Na pepo alipofukuzwa, yule bubu akasema, makutano wakastaajabu, wakanena, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.


Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.


Na aliposema haya, watu wote walioshindana nae wakatahayarika, mkutano wote wakafurahi kwa ajili ya mambo matukufu yaliyotendwa nae.


Makuhani wakuu na waandishi wakatafuta kumkamata saa hiyo hiyo, wakawaogopa watu: maana walitambua ya kuwa ule mfano amewanena wao.


Bali tukisema, Kwa wana Adamu, watu wote watatupiga mawe: kwa sababu wamesadiki ya kuwa Yohana ni nabii.


Makuhani wakuu na waandishi wakatafuta njia ya kumwua, kwa maana walikuwa wakiwaogopa watu.


Ushangao ukawashika wote wakamtukuza Mungu: wakajaa khofu, wakinena, Tumeona maajabu leo.


Lakini neno hili lisije likaenea katika watu, tuwaogofishe wasiseme tena na mtu aliye yote kwa jina hili.


maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arubaini.


na katika wote wengine hapana hatta mmoja aliyethubutu kuambatana nao: illa watu waliwaadhimisha:


Yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawatupia mawe.


Wakakubali maneno yake; wakawaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kiisha wakawaacha waende zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo