Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 4:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuukhubiri ufufuo wa wafu unaopatikana kwa Yesu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Walikasirika sana, maana hao mitume walikuwa wanawahubiria watu kwamba Yesu alifufuka, jambo ambalo linaonesha wazi kwamba wafu watafufuka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Walikasirika sana, maana hao mitume walikuwa wanawahubiria watu kwamba Yesu alifufuka, jambo ambalo linaonesha wazi kwamba wafu watafufuka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Walikasirika sana, maana hao mitume walikuwa wanawahubiria watu kwamba Yesu alifufuka, jambo ambalo linaonesha wazi kwamba wafu watafufuka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 huku wakiwa wamekasirika sana kwa sababu mitume walikuwa wanawafundisha watu na kuhubiri kwamba kuna ufufuo wa wafu ndani ya Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 huku wakiwa wamekasirika sana kwa sababu mitume walikuwa wanawafundisha watu na kuhubiri kwamba kuna ufufuo wa wafu ndani ya Isa.

Tazama sura Nakili

Matendo 4:2
18 Marejeleo ya Msalaba  

Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.

Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo.

Hatta wakati huo kukatukia ghasia si haba katika khabari ya Njia ile.

isipokuwa kwa ajili ya sauti hii moja, nilipolia nikisimama katikati yao, Kwa ajili ya ufufuo wa wafu ninahukumiwa mbele yenu hivi leo.

ya kwamba Kristo hana buddi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza khabari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa mataifa.

Kwa nini limedhaniwa nanyi kuwa neno lisilosadikika, kwamba Mungu awafufua wafu?

mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambae Mungu amemfufua: na sisi tu mashahidi wake.

Akaondoka kuhani mkuu na wote waliokuwa pamoja nae (hao ndio walio wa madhehehu ya Masadukayo) wamejaa wivu,

Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.

Lakini killa mmoja mahali pake; limbuko Kristo; baadae walio wake Kristo, atakapokuja.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo