Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 4:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Hao wazee wa Baraza, wakiwa wanajua kwamba Petro na Yohane walikuwa watu wasio na kisomo wala elimu yoyote, walishangaa juu ya jinsi walivyosema kwa uhodari. Wakatambua kwamba walikuwa wamejiunga na Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Hao wazee wa Baraza, wakiwa wanajua kwamba Petro na Yohane walikuwa watu wasio na kisomo wala elimu yoyote, walishangaa juu ya jinsi walivyosema kwa uhodari. Wakatambua kwamba walikuwa wamejiunga na Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Hao wazee wa Baraza, wakiwa wanajua kwamba Petro na Yohane walikuwa watu wasio na kisomo wala elimu yoyote, walishangaa juu ya jinsi walivyosema kwa uhodari. Wakatambua kwamba walikuwa wamejiunga na Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Viongozi na wazee walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa walikuwa watu wa kawaida, wasio na elimu, walishangaa sana, wakatambua kwamba hawa watu walikuwa na Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Wale viongozi na wazee walipoona ujasiri wa Petro na Yohana na kujua ya kuwa walikuwa watu wa kawaida, wasio na elimu, walishangaa sana, wakatambua kwamba hawa watu walikuwa na Isa.

Tazama sura Nakili




Matendo 4:13
22 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Alipotoka nje hatta ukumbini, mwanamke mwingine akamwona, akawaambia watu waliokuwa huko, Na huyu nae alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.


Punde kidogo, wale waliosimama karibu wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika na wewe u mmoja wao; maana hatta usemi wako wakutambulisha.


Akapeleka Petro na Yohana, akisema, Enendeni, mkatuandikie pasaka, illi tuile.


Bassi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, akamwambia mama yake, Bibi, tazama, mwana wako.


Wayahudi wakastaajabu, wakinena, Amepataje huyo kujua elimu, nae hajasoma?


Lakini makutano hayo wasioifahamu torati wamelaaniwa.


Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu.


Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia,


Bassi sasa, Bwana, yaangalie maogofya yao; ukawajalie watumishi wako kunena neno lako kwa uthabiti,


Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.


Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema nae, na jinsi alivyokhubiri pasipo khofu katika Dameski kwa jina lake Yesu.


Nae akawa pamoja nao katika Yerusalemi akiingia na kutoka.


bali Mungu aliyachagua mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena alivichagua vitu dhaifu vya dunia illi wenye nguvu waaibishwe;


na hivyo siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo, akianguka kifudifudi, atamwabudu Mungu, akikiri ya kuwa Mungu yu kati yenu hila shaka.


Bassi, kwa kuwa tuna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo