Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 3:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Kwa maana Musa aliwaambia baba zetu ya kama, Bwana Mungu atawainulieni nabii, atakaetoka katika ndugu zenu, kama mimi, msikieni yeye katika mambo yote atakayonena.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu nyinyi wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu nyinyi wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Kwa maana Mose alisema, ‘Bwana Mungu wenu atawapelekeeni nabii kama mimi kutoka kati yenu nyinyi wenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Kwa maana Musa alisema, ‘Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Itawapasa kumtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Kwa maana Musa alisema, ‘Bwana Mwenyezi Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Itawapasa kumtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia.

Tazama sura Nakili




Matendo 3:22
22 Marejeleo ya Msalaba  

Makutano wakanena, Huyu ni Yesu, yule nabii wa Nazareti ya Galilaya.


Illakini imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa, kwa maana haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemi.


Akawaambia, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu Mnazareti, aliyekuwa mtu nabii mwenye nguvu kwa tendo na kwa neno mbele za Mungu na watu wote;


Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo.


Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


Musa huyo ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii katika ndugu zenu, kama mimi: mtamsikia huyo.


Maana yale yasiyowezekana kwa sharia, kwa kuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwana wake mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa ajili ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili:


na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin.


Hatta ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwana wake, amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sharia,


KWA hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi yaliyasikiwa tusije tukayakosa.


nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo