Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 3:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Tubuni bassi, mrejee, illi dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuhurudishwa kwa kuwako kwake Bwana:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Basi, tubuni, mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Basi, tubuni, mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Basi, tubuni, mkamrudie Mungu ili yeye afute dhambi zenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Tubuni basi mkamgeukie Mungu, dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kutoka kwake Mwenyezi Mungu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Tubuni basi mkamgeukie Mwenyezi Mungu, dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Mwenyezi Mungu,

Tazama sura Nakili




Matendo 3:19
73 Marejeleo ya Msalaba  

Maana moyo wa watu hawa umekuwa mzito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao Wakasikia kwa masikio yao, Wakafahama kwa mioyo yao, Wakaongoka, Nikawaponya.


akasema, Amin, nawaambieni, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kabisa katika ufalme wa mbinguni.


Na wengi katika wana wa Israeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.


Akakana, akisema, Mwanamke, simjui.


Bassi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Bwana, wakati huu ndipo unapomrudishia Israeli ufalme wake?


Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.


Mkono wa Bwana ukawa pamoja nao: watu wengi wakaamini, wakamwelekea Bwana.


Bassi, wakisafirishwa na Kanisa, wakapita kati ya inchi ya Foiniki na Samaria, wakitangaza khabari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.


Nae alifanya killa taifa ya wana Adamu kuwa wa damu moja, wakae juu ya uso wa inchi yote, akiisha kuwaandikia nyakati alizowaamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


Kwa maana mioyo ya watu hawa imepumbaa, Na masikio yao ni wazito wa kusikia, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Na kusikia kwa masikio yao, Na kufahamu kwa mioyo yao, Na kuhadili nia zao Nikawaponya.


apate kumtuma Kristo aliyekhubiriwa kwenu tangu zamani;


ambae ilimpasa kupokewa mbinguni hatta zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake tokea mwanzo wa ulimwengu.


Kwa maana sitaki ndugu msiijue siri hii, ms jione kuwa wenye akili, ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka ntimilifu wa mataifa uwasili;


atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile.


na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,


akiwaonya kwai npole washindanao nae, illi, kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na ujuzi wa kweli,


BASSI, ikiwa ikaliko abadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.


Kwa maana mlikuwa kama kondoo wanaopotea; lakini sasa mmemrudia Mchunga na Askofu wa roho zenu.


Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu kama siku moja.


Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo