Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 3:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Na kwa imani ya jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnaemwona na kumjua: na imani ile iliyo kwa njia yake yeye imempatia huyu mbele yemi ninyi nyote uzima huu mkamilifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Jina la Yesu na imani katika jina hilo ndivyo vilivyompa nguvu mtu huyu mnayemwona na kumfahamu. Imani kwa Yesu ndiyo iliyomponya kabisa mtu huyu kama mnavyoona nyote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kwa imani katika jina la Isa, huyu mtu mnayemwona na kumfahamu ametiwa nguvu. Ni jina la Isa na imani kutoka kwake ambayo imemponya kabisa huyu mtu, kama nyote mnavyoona.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kwa imani katika jina la Isa, huyu mtu mnayemwona na kumfahamu ametiwa nguvu. Ni kwa jina la Isa na imani itokayo kwake ambayo imemponya kabisa huyu mtu, kama ninyi wote mnavyoona.

Tazama sura Nakili




Matendo 3:16
21 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akatembea juu ya maji, illi kumwendea Yesu.


Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile.


Amin, amin, nawaambieni, Aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi na yeye atazifanya; atafanya na kubwa kuliko hizi, kwa kuwa nashika njia kwenda kwa Baba.


Bassi ikiwa mtu apashwa tohara siku ya sabato, torati ya Musa isije ikavunjika, mbona mnanikasirikia kwa sababu nalimfanya mtu kuwa mzima kabisa siku ya sabato?


Mtu huyo alimsikia Paolo akinena; nae akamkazia macho akaona ya kuwa ana imani ya kuponywa,


Akawa akifanya hayo siku nyingi. Lakini Paolo akakasirika akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.


Petro akanena, Fedha sina, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Mnazareti, simama uende.


Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda: akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka, akimsifu Mungu.


jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu.


ukinyosha mkono wako kuponya: ishara na maajabu zifanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.


Wakawaweka katikati, wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani mmefanya haya ninyi?


ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.


Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama simi upendo, si kitu mimi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo