Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 3:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa ameketi na kuomba sadaka penye mlango mzuri wa hekalu: wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule “Mlango Mzuri” wa hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule “Mlango Mzuri” wa hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Walipomtambua kuwa ndiye yule aliyekuwa anaombaomba karibu na ule “Mlango Mzuri” wa hekalu, wakashangaa mno hata wasiweze kuelewa yaliyompata.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 wakamtambua kuwa ni yule mtu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango liitwalo Zuri akiomba msaada, nao wakajawa na mshangao, wakastaajabu kwa yale yaliyomtukia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 wakamtambua kuwa ni yule mtu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango liitwalo Zuri akiomba msaada, nao wakajawa na mshangao, wakastaajabu juu ya yale yaliyomtukia.

Tazama sura Nakili




Matendo 3:10
12 Marejeleo ya Msalaba  

Na watu wa mahali pale walipomtambua, wakatuma watu kwenda inchi zile zote zilizo kandokando, wakamletea wote waliokuwa hawawezi;


Ushangao ukawashika wote, wakaambiana wao kwa wao, wakinena, Neno gani hili, maana kwa mamlaka na uweza awaamuru pepo wachafu, nao watoka?


Watu wote wakashangaa kwa adhama yake Mungu. Hatta wote walipokuwa wakistaajabia mambo yote aliyoyafanya akawaambia wanafunzi wake,


Maana Baba ampenda Mwana, amwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; na kazi kubwa zaidi kuliko hizi atamwonyesha illi ninyi mpate kustaajabu.


Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe kwake.


Bassi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni kipofu, wakanena, Je! huyu siye yule aliyekuwa akiomba, ameketi?


Wakashangaa wote wakaingiwa na mashaka, wakaambiana, Maana yake nini mambo haya?


Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Si hawa wote wasemao Wagalilaya?


Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mama yake alichukuliwa na watu, wakamweka killa siku katika mlango wa hekalu nitwao Mzuri, illi aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo