Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 28:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Ikawa baba yake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paolo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, akamponya

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Basi, ikawa kwamba baba yake Publio alikuwa amelala kitandani, mgonjwa wa homa na kuhara. Paulo alikwenda kumwona na baada ya kusali, akaweka mikono yake juu ya mgonjwa, akamponya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Basi, ikawa kwamba baba yake Publio alikuwa amelala kitandani, mgonjwa wa homa na kuhara. Paulo alikwenda kumwona na baada ya kusali, akaweka mikono yake juu ya mgonjwa, akamponya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Basi, ikawa kwamba baba yake Publio alikuwa amelala kitandani, mgonjwa wa homa na kuhara. Paulo alikwenda kumwona na baada ya kusali, akaweka mikono yake juu ya mgonjwa, akamponya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Baba yake Publio alikuwa mgonjwa kitandani, akiwa anaugua homa na kuhara damu. Paulo akaingia ndani ili kumwona na baada ya maombi, akaweka mikono juu yake na kumponya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Baba yake Publio alikuwa mgonjwa kitandani, akiwa anaumwa homa na kuhara damu. Paulo akaingia ndani ili kumwona na baada ya maombi, akaweka mikono juu yake na kumponya.

Tazama sura Nakili




Matendo 28:8
22 Marejeleo ya Msalaba  

AKAWAITA wanafunzi wake thenashara, akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, wawafukuze, na kuponya magonjwa yote na dhaifu zote.


Ponyeni wagonjwa, takaseni wenye ukoma, fufueni wafu, fukuzeni pepo; mmepata burre, toeni burre.


Akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, nkawa mzima kama mkono wa pili.


Alipokuwa akiwaambia haya, yuaja jumbe mmoja, akamsujudia, akinena, Binti yangu udio kwanza afe: lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, uae atapona.


watashika nyoka; hatta wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.


akimsihi sana, akinena. Binti yangu mdogo yu katika kufa: nakuomba nje, nweke mkono wako juu yake, apate kupona, nae ataishi.


Wala hakuweza kufanya mwujiza wo wote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya.


Wakamletea kiziwi, nae ana kigugumizi, wakamsihi aweke mikono yake juu yake.


Akaweka mikono yake juu yake, akanyoka marra hiyo, akaanza kumtukuza Mungu.


Hatta jua lilipokuwa likichwa watu wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali wakawaleta kwake: nae akaweka mikono yake juu ya killa mmoja, akawaponya.


Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya mkubwa wa kisiwa, jina lake Publio; mtu huyu akatukaribisha kwa moyo wa urafiki, akatufanya wageni wake kwa muda wa siku tatu.


Yalipokwisha kutendeka hayo wengine waliokuwa na magonjwa katika kisiwa wakaja wakaponywa; nao wakatuheshimu kwa heshima nyingi.


Petro akawatoa wote, akapiga magoti, akaomba, akaielekea mayiti, akanena, Tabitha, ondoka. Nae akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.


Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kiisha miujiza, kiisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na kutawala, na aina za lugha.


mwingine imani katika Roho yule yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo