Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 28:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya mkubwa wa kisiwa, jina lake Publio; mtu huyu akatukaribisha kwa moyo wa urafiki, akatufanya wageni wake kwa muda wa siku tatu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya Publio, mkuu wa kile kisiwa. Publio alitukaribisha kirafiki, tukawa wageni wake kwa siku tatu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya Publio, mkuu wa kile kisiwa. Publio alitukaribisha kirafiki, tukawa wageni wake kwa siku tatu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Karibu na mahali pale palikuwa na mashamba ya Publio, mkuu wa kile kisiwa. Publio alitukaribisha kirafiki, tukawa wageni wake kwa siku tatu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Basi karibu na sehemu ile, palikuwa na shamba kubwa la kiongozi mkuu wa kile kisiwa, aliyeitwa Publio. Alitupokea kwake, na akatuhudumia kwa ukarimu mkubwa kwa muda wa siku tatu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Basi karibu na sehemu ile, palikuwa na shamba kubwa la mtu mmoja kiongozi wa kile kisiwa, aliyeitwa Publio. Alitupokea na akatuhudumia kwa ukarimu mkubwa kwa muda wa siku tatu.

Tazama sura Nakili




Matendo 28:7
10 Marejeleo ya Msalaba  

mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paolo, mtu mwenye akili. Yeye akawaita Barnaba na Saul waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu.


Hatta Gallio alipokuwa Prokonsuli wa Akaya, Wayahudi wakamwendea Paolo kwa nia moja, wakamleta mbele ya kiti cha hukumu,


Akawaambia kuweka nyama tayari wampandishe Paolo, na kumchukua salama kwa Feliki liwali.


Washenzi wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana walikoka moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyokunywa na kwa sababu ya baridi.


Wakamwangalia sana wakidhani ya kuwa atavimba au kuanguka chini, amekwisha kufa kwa ghafula; na wakiisha kumwangalia sana, na kuona kwamba halimpati dhara lo lote, wakabadili fikara zao, wakasema kwamba yeye ni Mungu.


Ikawa baba yake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paolo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, akamponya


na kushuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata killa tendo jema.


Msisahau kuwafadhilia wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo