Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 28:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Paolo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka juu ya moto, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto, akamzingisha katika mkono wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Paulo aliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitia motoni. Hapo, kwa sababu ya lile joto la moto, nyoka akatoka katika kuni akamnasa Paulo mkononi na kujishikilia hapo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Paulo aliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitia motoni. Hapo, kwa sababu ya lile joto la moto, nyoka akatoka katika kuni akamnasa Paulo mkononi na kujishikilia hapo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Paulo aliokota mzigo mdogo wa kuni akawa anazitia motoni. Hapo, kwa sababu ya lile joto la moto, nyoka akatoka katika kuni akamnasa Paulo mkononi na kujishikilia hapo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Paulo alikusanya mzigo wa kuni, na alipokuwa anaweka kuni kwenye moto, nyoka mwenye sumu akatoka humo kwa ajili ya joto na kujisokotea mkononi mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Paulo alikuwa amekusanya mzigo wa kuni na alipokuwa anaweka kwenye moto kwa ajili ya joto, nyoka mwenye sumu akatoka humo na kujisokotea mkononi mwake.

Tazama sura Nakili




Matendo 28:3
13 Marejeleo ya Msalaba  

Uzao wa nyoka, mwawezaje kusema mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.


Enyi nyoka, mazao wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum?


Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo?


watashika nyoka; hatta wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.


Washenzi wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana walikoka moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyokunywa na kwa sababu ya baridi.


Washenzi walipomwona yule nyoka akimwangikia mkono, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni muuaji; na ijapokuwa ameokoka katika bahari, haki haimwachi kuishi.


Wao wakhudumu wa Kristo? (nanena kiwazimu), mimi zaidi; kwa kazi kuzidi sana; kwa mapigo kupita kiasi; kwa vifungo kuzidi sana; kwa mauti marra nyingi.


kama wasiojulika, bali wajulikao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hayi; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo