Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 28:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Bassi ijulikane kwenu ya kwamba wokofu huu wa Mungu umepelekwa kwa mataifa, nao watasikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Halafu Paulo akasema, “Jueni basi, kwamba ujumbe wa Mungu juu ya wokovu umepelekwa kwa watu wa mataifa. Wao watasikiliza!” [

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Halafu Paulo akasema, “Jueni basi, kwamba ujumbe wa Mungu juu ya wokovu umepelekwa kwa watu wa mataifa. Wao watasikiliza!” [

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Halafu Paulo akasema, “Jueni basi, kwamba ujumbe wa Mungu juu ya wokovu umepelekwa kwa watu wa mataifa. Wao watasikiliza!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 “Basi na ijulikane kwenu kwamba, huu wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa Mataifa, nao watasikiliza.” [

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 “Basi na ijulikane kwenu kwamba, huu wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa Mataifa, nao watasikiliza.” [

Tazama sura Nakili




Matendo 28:28
26 Marejeleo ya Msalaba  

Na wote wenye mwili watanona wokofu wa Mungu.


Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.


Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, nao miongoni mwenu mnaomcha Mungu, kwenu ninyi neno la wokofu huu limepelekwa.


Bassi, ibainike kwenu, ndugu, ya kuwa kwa huyu mnakhubiriwa ondoleo la dhambi;


Hatta walipolika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwaruba amewafungulia mataifa mlango wa imani.


Simeon ametueleza jinsi Mungu alivyowaangalia mataifa illi achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake.


Illi wana Adamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao: Asema Bwana afanyae mambo haya yote.


Walipopingamana nae na kutukana, akakungʼuta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu: mimi ni safi: langu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.


Lakini Petro akasimama pamoja na wale edashara, akapaaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemi, jambo hili lijulike kwenu, mkasikilize maneno yangu.


Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.


Alipokwisha kusema haya, Wayahudi wakaenda zao, wakiulizana mengi wao kwa wao.


jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Mnazareti, ambae ninyi mlimsulibisha, Mungu akamfufua, kwa jina hilo mtu huyu anasimama mzima mbele yenu.


Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


Bassi nasema, Je! wamejikwaa hatta wameanguka kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokofu umewafikilia mataifa, illi wao watiwe wivu:


Nae aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya wema wa imani aliyokuwa nayo kabla asijatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, illi na wao pia wahesahiwe wema;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo