Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 28:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Wale wakamwambia, Sisi hatukupata nyaraka zenye khabari zako kutoka Yahudi, wala hapana ndugu hatta mmoja aliyefika hapa na kutupasha khabari, au kunena neno baya juu yako.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Wao wakamwambia, “Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea, wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa na kutoa habari rasmi au kusema chochote kibaya juu yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Wao wakamwambia, “Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea, wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa na kutoa habari rasmi au kusema chochote kibaya juu yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Wao wakamwambia, “Sisi hatujapokea barua yoyote kutoka Yudea, wala hakuna ndugu yeyote aliyefika hapa na kutoa habari rasmi au kusema chochote kibaya juu yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Wakamjibu, “Hatujapokea barua zozote kutoka Yudea zinazokuhusu, wala hapana ndugu yeyote aliyekuja hapa ambaye ametoa taarifa au kuzungumza jambo lolote baya juu yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Wakamjibu, “Hatujapokea barua zozote kutoka Uyahudi zinazokuhusu, wala hapana ndugu yeyote aliyekuja hapa ambaye ametoa taarifa au kuzungumza jambo lolote baya juu yako.

Tazama sura Nakili

Matendo 28:21
8 Marejeleo ya Msalaba  

Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.

Huko tukakuta ndugu, tukasihiwa nao tukae siku saba; na hivi tukafika Rumi.

Bassi sasa ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda.

Kwa maana naliomba mimi mwenyewe niharamishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo