Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 28:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Washenzi wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana walikoka moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyokunywa na kwa sababu ya baridi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Wenyeji wa hapo walikuwa wema sana kwetu. Mvua ilikuwa inaanza kunyesha na kulikuwa na baridi, hivyo waliwasha moto, wakatukaribisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Wenyeji wa hapo walikuwa wema sana kwetu. Mvua ilikuwa inaanza kunyesha na kulikuwa na baridi, hivyo waliwasha moto, wakatukaribisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Wenyeji wa hapo walikuwa wema sana kwetu. Mvua ilikuwa inaanza kunyesha na kulikuwa na baridi, hivyo waliwasha moto, wakatukaribisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Wenyeji wa kile kisiwa walituonesha ukarimu usio wa kawaida. Waliwasha moto na kutukaribisha sisi sote kwa sababu mvua ilikuwa inanyesha na kulikuwa na baridi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Wenyeji wa kile kisiwa wakatufanyia ukarimu usio wa kawaida. Waliwasha moto na kutukaribisha sisi sote kwa sababu mvua ilikuwa inanyesha na kulikuwa na baridi.

Tazama sura Nakili




Matendo 28:2
19 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtu aliye yote atakaemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa kikombe cha maji ya baridi tu, kwa kuwa yu mwanafunzi, amin, nawaambieni, haitampotea kamwe thawabu yake.


Na wale watumishi na askari walikuwa wamesimama, wamefanya moto wa makaa; maana ilikuwa baridi, wakawa wakikota moto. Petro nae, alikuwa pamoja nao, anakota moto.


Siku ya pili tukawasili Sidon; Yulio akamfadhili sana Paolo akampa rukhusa kwenda kwa rafiki zake, kutunzwa nao.


Paolo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni, na kuuweka juu ya moto, nyoka akatoka kwa ajili ya ule moto, akamzingisha katika mkono wake.


Washenzi walipomwona yule nyoka akimwangikia mkono, wakaambiana, Hakosi mtu huyu ni muuaji; na ijapokuwa ameokoka katika bahari, haki haimwachi kuishi.


Nawiwa na Wayunani na washenzi, nawiwa na wenye hekima na wajinga.


LAKINI yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, illakini msimhukumu mawazo yake.


Yeye alae asimdharau yeye asiyekula, nae asiyekula asimhukumu yeye alae; kwa maana Mungu amemkubali.


Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati?


Bassi nisipojua maana ya ile sauti nitakuwa mshenzi kwake yeye anenae; nae atakuwa mshenzi kwangu.


kwa kazi na kusumbuka; kwa kukesha marra nyingi; kwa njaa na kiu; kwa kufunga marra nyingi; kwa baridi na kuwa uchi.


Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mshenzi wala Mskuthi, mtumwa wala mungwana, bali Kristo ni yote, na katika wote.


Msisahau kuwafadhilia wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo