Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 28:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane; hatta walipokuja akawaambia, Wanaume ndugu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, nimefungwa, tokea Yerusalemi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Baada ya siku tatu, Paulo aliwaita pamoja viongozi wa Kiyahudi wa mahali hapo. Walipokusanyika, Paulo aliwaambia, “Wananchi wenzangu, mimi, ingawa sikufanya chochote kibaya wala kupinga desturi za wazee wetu, nilitiwa nguvuni kule Yerusalemu na kutiwa mikononi mwa Waroma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Baada ya siku tatu, Paulo aliwaita pamoja viongozi wa Kiyahudi wa mahali hapo. Walipokusanyika, Paulo aliwaambia, “Wananchi wenzangu, mimi, ingawa sikufanya chochote kibaya wala kupinga desturi za wazee wetu, nilitiwa nguvuni kule Yerusalemu na kutiwa mikononi mwa Waroma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Siku tatu baadaye Paulo akawaita pamoja viongozi wa Wayahudi. Walipokwisha kukusanyika akawaambia, “Ndugu zangu, ingawa sikufanya jambo lolote dhidi ya watu wetu au dhidi ya desturi za baba zetu, lakini nilikamatwa huko Yerusalemu nikakabidhiwa kwa Warumi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Siku tatu baadaye Paulo akawaita pamoja viongozi wa Kiyahudi. Walipokwisha kukusanyika akawaambia, “Ndugu zangu, ingawa sikufanya jambo lolote dhidi ya watu wetu au dhidi ya desturi za baba zetu, lakini nilikamatwa huko Yerusalemu nikakabidhiwa kwa Warumi.

Tazama sura Nakili

Matendo 28:17
11 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watawa na watu wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paolo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.

Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.

Na wale walipofika Kaisaria, wakampa liwali ile barua, wakamweka Paolo mbele yake. Nae alipokwislia kuisoma, akawauliza, Mtu huyu ni wa wilaya gani?

Paolo akasema, Mimi ninasimama hapa mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari, panipasapo kuhukumiwa: sikuwakosa Wayahudi neno, kama wewe ujuavyo sana.

Kuhani mkuu na Wayahudi wakampasha khabari za Paolo, wakamsihi,

Paolo akajitetea hivi, ya kama, Mimi sikukosa neno juu ya sharia ya Wayahudi, wiila juu ya hekalu wala juu ya Kaisari.

maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu pahali hapa, na kuzihadili desturi tulizopewa na Musa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo