Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 28:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Tulipoingia Rumi akida akawatia wafungwa katika mikono ya jemadari wa walinzi wa Praitorio: bali Paolo alipewa rukhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Tulipofika Roma, Paulo aliruhusiwa kukaa peke yake pamoja na askari mmoja wa kumlinda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Tulipofika Roma, Paulo aliruhusiwa kukaa peke yake pamoja na askari mmoja wa kumlinda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Tulipofika Roma, Paulo aliruhusiwa kukaa peke yake pamoja na askari mmoja wa kumlinda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Tulipofika Rumi, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake akiwa na askari wa kumlinda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Tulipofika Rumi, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake akiwa na askari wa kumlinda.

Tazama sura Nakili




Matendo 28:16
18 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akula, mzalia wa Ponto; nae amekuja kutoka inchi ya italia siku za karibu, pamoja na Priskilla mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi.


Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.


Frugia na Pamfulia, Misri na pande za Libua karibu na Kurene, na Warumi wageni, Wayahudi na Waongofu,


Usiku ule Bwana akasimama karibu nae, akasema, Uwe na moyo mkuu, Paolo; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia khabari zangu Yerusalemi, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi.


Akamwamuru yule akida amlinde Paolo; illa awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumkhudumu au kuja kumtazama.


Siku ya pili tukawasili Sidon; Yulio akamfadhili sana Paolo akampa rukhusa kwenda kwa rafiki zake, kutunzwa nao.


Paolo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya marikebu hamtaweza kuokoka.


Bali akida, akitaka kumponya Paolo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe baharini, wafike inchi kavu;


Na yule mwanamke uliyemwona, ndiye mji ule mkubwa, mwenye ufalme juu ya wafalme wa inchi.


Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke yule.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo