Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 28:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Na kutoka huko ndugu, waliposikia khabari zetu, wakaja kutulaki mpaka Appiiforo na Trestaberne. Paolo alipowaona akamshukuru Mungu, akachangaʼmka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Ndugu wa kule Roma walipopata habari zetu, wakaja kutulaki kwenye soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, akapata moyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Ndugu wa kule Roma walipopata habari zetu, wakaja kutulaki kwenye soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, akapata moyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Ndugu wa kule Roma walipopata habari zetu, wakaja kutulaki kwenye soko la Apio na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona alimshukuru Mungu, akapata moyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Ndugu wa huko Rumi waliposikia habari zetu, walikuja hadi Soko la Apio na mahali paitwapo Mikahawa Mitatu kutulaki. Paulo alipowaona, alimshukuru Mungu akatiwa moyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Ndugu wa huko Rumi waliposikia habari zetu, walikuja mpaka Soko la Apio na mahali paitwapo Mikahawa Mitatu kutulaki. Paulo alipowaona, alimshukuru Mungu akatiwa moyo.

Tazama sura Nakili




Matendo 28:15
22 Marejeleo ya Msalaba  

wakatwaa matawi ya mitende wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana; Amebarikiwa ajiie kwa jina la Bwana, mfalme wa Israeli.


Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


Akasema, Ingieni; akawakaribisha. Hatta siku ya pili, Petro akatoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu waliokaa Yoppa wakafuatana nae.


Petro alipokuwa akiingia, Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia.


BASSI mitume na ndugu waliokuwa katika Yahudi wakapata khabari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Bwana.


Roho akaniambia nifuatane nao, nisione mashaka. Ndugu hawa sita nao wakaenda pamoja nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule:


Nae akawapungia mkono wanyamaze, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa katika gereza. Akasema, Enendeni, mkampashe Yakobo na ndugu zetu khabari hizi. Akaondoka, akaenda mahali pengine.


Hatta tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote pamoja na wake zao na watoto wao wakatusindikiza hatta nje ya mji, wakapiga magoti pwani wakaomba:


Huko tukakuta ndugu, tukasihiwa nao tukae siku saba; na hivi tukafika Rumi.


wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Hispania nitakuja kwenu, kwa maana nataraja kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kupelekwa mbele nanyi, moyo wangu ushibe kwenu ijapokuwa ni kidogo.


Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.


na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu, kama Yesu Kristo.


kwa sababu hiyo tulifarijiwa, ndugu, kwa khabari zenu, katika shidda na mateso yetu yote, kwa imani yenu.


Wakumbukeni waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; nao wanaodhulumiwa, kwa kuwa nanyi m katika mwili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo