Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 27:43 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

43 Bali akida, akitaka kumponya Paolo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe baharini, wafike inchi kavu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

43 Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitaka kumwokoa Paulo, aliwazuia wasifanye hivyo. Aliamuru wale waliojua kuogelea waruke kutoka melini na kuogelea hadi pwani,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

43 Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitaka kumwokoa Paulo, aliwazuia wasifanye hivyo. Aliamuru wale waliojua kuogelea waruke kutoka melini na kuogelea hadi pwani,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

43 Lakini kwa vile yule ofisajeshi alitaka kumwokoa Paulo, aliwazuia wasifanye hivyo. Aliamuru wale waliojua kuogelea waruke kutoka melini na kuogelea hadi pwani,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

43 Lakini yule jemadari alitaka kuokoa maisha ya Paulo, basi akawazuia askari wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, waogelee hadi nchi kavu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

43 Lakini yule jemadari alitaka kuokoa maisha ya Paulo, basi akawazuia askari wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, waogelee mpaka nchi kavu.

Tazama sura Nakili




Matendo 27:43
8 Marejeleo ya Msalaba  

Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paolo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumpokonya mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.


Akawaambia kuweka nyama tayari wampandishe Paolo, na kumchukua salama kwa Feliki liwali.


Lakini yule akida akawasikiliza nakhodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paolo.


Siku ya pili tukawasili Sidon; Yulio akamfadhili sana Paolo akampa rukhusa kwenda kwa rafiki zake, kutunzwa nao.


Paolo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya marikebu hamtaweza kuokoka.


Shauri la askari lilikuwa wafungwa wauawe, mtu asiogelee na kukimbia.


Marra tatu nalipigwa bakora; marra moja nalipigwa mawe; marra tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo