Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 27:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 Alipokwisha kusema haya akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Baada ya kusema hivyo, Paulo alichukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega, akaanza kula.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Baada ya kusema hivyo, Paulo alichukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega, akaanza kula.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Baada ya kusema hivyo, Paulo alichukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega, akaanza kula.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Baada ya kusema maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Baada ya kusema maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula.

Tazama sura Nakili




Matendo 27:35
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akamega, akawapa wanafunzi ile mikate, wanafunzi wakawapa makutano.


akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru, akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.


Akawaagiza makutano waketi chini: akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandalie: wakawaandalia makutano,


Ikawa, akiketi pamoja nao, akautwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawagawia.


Bassi Yesu akaitwaa mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka.


(lakini mashua nyingine zilikuja kutoka Tiberia karibu na pahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aiiposhukuru);


kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.


Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu.


Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.


Bassi usiutahayarikie ushuhuda wa Bwana wetu, wala mimi mtumwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja na Injili kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;


Illakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo