Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 27:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Usiogope, Paolo, huna buddi kusimama mbele ya Kaisari: tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 akaniambia: ‘Paulo, usiogope! Ni lazima utasimama mbele ya Kaisari; naye Mungu, kwa wema wake, amekufadhili kwa kuwaokoa wote wanaosafiri nawe wasiangamie.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 akaniambia: ‘Paulo, usiogope! Ni lazima utasimama mbele ya Kaisari; naye Mungu, kwa wema wake, amekufadhili kwa kuwaokoa wote wanaosafiri nawe wasiangamie.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 akaniambia: ‘Paulo, usiogope! Ni lazima utasimama mbele ya Kaisari; naye Mungu, kwa wema wake, amekufadhili kwa kuwaokoa wote wanaosafiri nawe wasiangamie.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 akaniambia, ‘Paulo usiogope, kwa kuwa ni lazima usimame mbele ya Kaisari, naye Mungu amekupa kwa neema uhai wa wote wanaosafiri pamoja nawe.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 naye akasema, ‘Paulo usiogope, kwa kuwa ni lazima usimame mbele ya Kaisari, naye Mungu amekupa kwa neema uhai wa wote wanaosafiri pamoja nawe.

Tazama sura Nakili




Matendo 27:24
35 Marejeleo ya Msalaba  

nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, illi kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.


Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho: afadhali mmwogopeni yule awezae kuangamiza mwili na roho pia katika jehannum.


Yesu akajibu, Saa za mchana je si thenashara? Mtu akienda mchana hajikwai, kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.


Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.


Usiku ule Bwana akasimama karibu nae, akasema, Uwe na moyo mkuu, Paolo; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia khabari zangu Yerusalemi, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi.


Ikiwa nimekosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; hali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezae kunitia mikononi mwao. Nataka rufaani kwa Kaisari.


Paolo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya marikebu hamtaweza kuokoka.


Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu miateen na sabaini na sita.


Shauri la askari lilikuwa wafungwa wauawe, mtu asiogelee na kukimbia.


nao waliosalia, hawa juu ya mbao na hawa juu ya vitu vingine vya merikebu. Na hivyo watu wote wakapata kuifikia inchi kavu salama.


Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa: maana nataraja ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata.


Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.


Na nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akiniambia, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo