Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 27:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Na tulipokuwa tumekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paolo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, ingalikuwa kheri kama mngalinisikiliza na kutokungʼoa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Baada ya kukaa muda mrefu bila kula chakula, Paulo alisimama kati yao, akasema, “Waheshimiwa, ingalikuwa afadhali kama mngalinisikiliza na kuacha kusafiri kutoka Krete. Kama mngalifanya hivyo tungaliiepuka shida hii na hasara hizi zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Baada ya kukaa muda mrefu bila kula chakula, Paulo alisimama kati yao, akasema, “Waheshimiwa, ingalikuwa afadhali kama mngalinisikiliza na kuacha kusafiri kutoka Krete. Kama mngalifanya hivyo tungaliiepuka shida hii na hasara hizi zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Baada ya kukaa muda mrefu bila kula chakula, Paulo alisimama kati yao, akasema, “Waheshimiwa, ingalikuwa afadhali kama mngalinisikiliza na kuacha kusafiri kutoka Krete. Kama mngalifanya hivyo tungaliiepuka shida hii na hasara hizi zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Baada ya watu kukaa siku nyingi bila kula chakula, Paulo akasimama mbele yao na kusema: “Enyi watu, kama mngekubali ushauri wangu wa kutosafiri kwa meli kutoka Krete, basi mngejiepusha na uharibifu na hasara hii.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Baada ya watu kukaa siku nyingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati yao akasema, “Enyi watu, iliwapasa kunisikiliza na kuacha kusafiri baharini kutoka Krete, ndipo ninyi mngekuwa mmejinusuru na uharibifu huu na hasara hii.

Tazama sura Nakili

Matendo 27:21
8 Marejeleo ya Msalaba  

Na kwa sababu bandari haikukaa vema, watu wakae ndani yake wakati wa haridi, walio wengi wakatoa shauri tutweke tukatoke huko illi wapate kufika Foiniki, kama ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi: nayo ni bandari ya Krete, inaelekea kaskazini-mashariki na kusini-mashariki.

Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata walioazimu kupata, wakangʼoa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani.

Na jua na nyota hazikuonekana kwa muda wa siku nyingi, na tufani kuu ikatushika, bassi tukakata tamaa ya kuokoka.

Tukasafiri pole pole kwa muda wa siku nyingi, tukafika hatta Knido kwa shidda; na kwa sababu upepo ulikuwa ukituzuia tukapita chini ya Krete illi kuukinga upepo, tukaikabili Salmone.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo