Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 27:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Tukapanda katika merikebu ya Adramuttio iliyokuwa tayari kusafiri hatta miji ya pwani za Asia, tukatweka; Aristarko, Mmakedoni wa Thessalonika, akiwa pamoja nasi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Tulipanda meli ya Adiramito iliyokuwa inasafiri na kupitia bandari kadhaa za mkoa wa Asia, tukaanza safari. Aristarko, mwenyeji wa Makedonia kutoka Thesalonike, alikuwa pamoja nasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Tulipanda meli ya Adiramito iliyokuwa inasafiri na kupitia bandari kadhaa za mkoa wa Asia, tukaanza safari. Aristarko, mwenyeji wa Makedonia kutoka Thesalonike, alikuwa pamoja nasi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Tulipanda meli ya Adiramito iliyokuwa inasafiri na kupitia bandari kadhaa za mkoa wa Asia, tukaanza safari. Aristarko, mwenyeji wa Makedonia kutoka Thesalonike, alikuwa pamoja nasi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Tulipanda meli iliyotoka Adramitio, iliyokuwa inakaribia kusafiri kwenda kwenye bandari zilizopo pwani ya jimbo la Asia, tukaanza safari yetu tukiwa pamoja na Aristarko, Mmakedonia kutoka Thesalonike.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Tulipanda meli iliyotoka Adramitio, iliyokuwa inakaribia kusafiri kwenda kwenye bandari zilizopo pwani ya Asia, tukaanza safari yetu tukiwa pamoja na Aristarko, Mmakedonia kutoka Thesalonike.

Tazama sura Nakili




Matendo 27:2
17 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa siku mojawapo ya siku zile akapanda chomboni, yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu ya ziwa: wakatweka matanga.


Akamfuata Paolo na sisi, akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kutukhubiri njia ya wokofu.


WAKIISHA kupita kati ya Amfipoli na Apollonia wakafika Thessalonika, na hapo palikuwa na sunagogi la Wayahudi.


Na watu wengi katika wale waliotumia mambo ya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma moto mbele ya watu wote: wakafanya hesabu ya thamani yake wakaona ya kwamba yapata fedha khamsini elfu.


Mji wote ukajaa ghasia, wakaenda mbio wakaingia theatro kwa moyo mmoja, wakiisha kuwakamata Gaio na Aristarko, watu wa Makedonia waliosafiri pamoja na Paolo.


Waparthi na Wamedi na Waelamiti, nao wakaao Mesopotamia, Yahudi ua Kappadokia, Ponto na Asia,


Hatta tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote pamoja na wake zao na watoto wao wakatusindikiza hatta nje ya mji, wakapiga magoti pwani wakaomba:


Na tulipoondoka wakatupakilia vitu vile tulivyokuwa na haja navyo.


Tukafika Surakusa, tukakaa siku tatu.


Tulipoingia Rumi akida akawatia wafungwa katika mikono ya jemadari wa walinzi wa Praitorio: bali Paolo alipewa rukhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda.


Washenzi wakatufanyia fadhili zisizokuwa za kawaida. Kwa maana walikoka moto, wakatukaribisha sote, kwa sababu ya mvua iliyokunywa na kwa sababu ya baridi.


Aristarko, aliyefumgwa pamoja nami, awasalimu, na Marko, mjomba wake Barnaba, amhae mmepokea maagizo kwa khabari yake; akifika kwenu mkaribisheni.


na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo