Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 27:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Na upepo wa kusi ulipoanza kuvuma kidogo, wakidhani ya kuwa wamepata walioazimu kupata, wakangʼoa nanga, wakasafiri karibu na Krete pwani kwa pwani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakangoa nanga, wakaiendesha meli karibu sana na pwani ya Krete.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakangoa nanga, wakaiendesha meli karibu sana na pwani ya Krete.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Basi, upepo mzuri wa kusi ulianza kuvuma, nao wakadhani wamefanikiwa lengo lao; hivyo wakang'oa nanga, wakaiendesha meli karibu sana na pwani ya Krete.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Upepo mtulivu ulipoanza kuvuma toka kusini, wakadhani kuwa wangeweza kufikia lengo lao, hivyo wakang’oa nanga na kusafiri wakipita kandokando ya pwani ya kisiwa cha Krete.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Upepo mtulivu ulipoanza kuvuma toka kusini, wakadhani kuwa wangeweza kufikia lengo lao, hivyo wakang’oa nanga na kusafiri wakipita kandokando ya pwani ya kisiwa cha Krete.

Tazama sura Nakili




Matendo 27:13
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na killa ivumapo kaskazi mwasema, Itakuwa joto; ikawa.


Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa maneno yetu matendo makuu ya Mungu.


Na kwa sababu bandari haikukaa vema, watu wakae ndani yake wakati wa haridi, walio wengi wakatoa shauri tutweke tukatoke huko illi wapate kufika Foiniki, kama ikiwezekana, na kukaa huko wakati wa baridi: nayo ni bandari ya Krete, inaelekea kaskazini-mashariki na kusini-mashariki.


Na tulipokuwa tumekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paolo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, ingalikuwa kheri kama mngalinisikiliza na kutokungʼoa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii.


Tukaipita kwa shidda, pwani kwa pwani, tukafika mahali paitwapo Bandari Nzuri. Karibu na hapo pana mji uitwao Lasaya.


Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema. Wakrete ni wawongo siku zote, nyama mwitu wahaya, walafi, wasiofanya kazi. Ushuhuda huu ni kweli.


Kwa sababu hii nalikuaeba katika Krete, illi nyatengeneze yaliyosalia, na kuweka wazee katika killa mji kama nilivyokuamuru;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo