Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 27:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BASSI ilipoamriwa tusafiri hatta Italia, wakamtia Paolo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosi kiitwacho “Kikosi cha Augusto.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosi kiitwacho “Kikosi cha Augusto.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Walipokwisha amua tusafiri mpaka Italia, walimweka Paulo pamoja na wafungwa wengine chini ya ulinzi wa Yulio aliyekuwa ofisa wa jeshi katika kikosi kiitwacho “Kikosi cha Augusto.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ilipoamuliwa kwamba tungesafiri kwa meli kwenda Italia, Paulo na wafungwa wengine wakakabidhiwa kwa kiongozi mmoja wa askari aliyeitwa Juliasi, aliyekuwa wa Kikosi cha Walinzi wa Kaisari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ilipoamuliwa kwamba tungesafiri kwa njia ya bahari kwenda Italia, Paulo na wafungwa wengine wakakabidhiwa kwa kiongozi mmoja wa askari aliyeitwa Juliasi, aliyekuwa wa Kikosi cha Walinzi wa Kaisari.

Tazama sura Nakili




Matendo 27:1
29 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


Akida alipoona lililokuwa, akamtukuza Mungu, akisema, Kwa kweli mtu huyu alikuwa mwenye haki.


Na mtumishi wa akida mmoja alikuwa hawezi, karibu kufa, nae ni mtu aliyependwa nae sana.


PALIKUWA na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitaliano,


Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mcha Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno yako.


Bassi alipokwisha kuona yale maono, marra tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Bwana ametuita tuwakhubiri Injili.


Akamwona Myahudi mmoja, jina lake Akula, mzalia wa Ponto; nae amekuja kutoka inchi ya italia siku za karibu, pamoja na Priskilla mkewe, kwa sababu Klaudio amewaamuru Wayahudi wote watoke Rumi.


Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.


Marra hiyo akatwaa askari na maakida, akawashukia mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paolo.


Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? kwa maana mtu huyu ni Mrumi.


Usiku ule Bwana akasimama karibu nae, akasema, Uwe na moyo mkuu, Paolo; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia khabari zangu Yerusalemi, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi.


Paolo akamwita akida mmoja, akasema, Mchukue huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwarifu.


Akamwamuru yule akida amlinde Paolo; illa awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumkhudumu au kuja kumtazama.


Bassi Festo alipokwisha kusema na watu wa baraza, akajibu, Umetaka rufaani kwa Kaisari! bassi, utakwenda kwa Kaisari.


Nami nilipoona kama hakutenda neno la kustahili kuuawa, na yeye mwenyewe alipotaka kuhukumiwa na Augusto, nalikusudia kumpeleka kwake.


Lakini yule akida akawasikiliza nakhodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyoyasema Paolo.


Bali akida, akitaka kumponya Paolo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe baharini, wafike inchi kavu;


Na huko yule akida akakuta merikebu ya Iskanderia, tayari kusafiri hatta Italia, akatupandisha.


TULIPOKWISHA kuokoka, ndipo tukajua ya kuwa kisiwa kile chaitwa Melita.


Tulipoingia Rumi akida akawatia wafungwa katika mikono ya jemadari wa walinzi wa Praitorio: bali Paolo alipewa rukhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda.


Wasalimuni wote walio na mamlaka juu yenu, na watakatifu wote; walio wa Italia wanakusalimuni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo