Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 26:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Paolo akamjibu, Namwomba Mungu kwamba ikiwa kwa machache au ikiwa kwa mengi si wewe tu illa na hao wote wanaonisikia leo wawe kama mimi pasipo vifungo hivi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Paulo akamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi, lakini bila hii minyororo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Paulo akamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi, lakini bila hii minyororo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Paulo akamjibu, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu bali wote wanaonisikia leo wapate kuwa kama nilivyo mimi, lakini bila hii minyororo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Paulo akasema, “Ikiwa ni kwa haraka au la, namwomba Mungu, si wewe peke yako bali pia wale wote wanaonisikiliza leo, wawe kama mimi nilivyo, kasoro minyororo hii.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Paulo akasema, “Ikiwa ni kwa haraka au la, namwomba Mungu, si wewe peke yako bali pia wale wote wanaonisikiliza leo, wawe kama mimi nilivyo, kasoro minyororo hii.”

Tazama sura Nakili

Matendo 26:29
18 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mimi sipokei ushuhuda kwa wana Adamu; walakini ninasema haya illi ninyi mpate kuokoka.

Hatta wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule. Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili: walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.

Kiisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili: akauliza, Nani huyu? tena, amefanya nini?

Na walipokuwa wakikaa huko siku nyingi, Festo akamweleza mfalme khabari za Paolo, akisema, Yupo hapa mtu aliyeachwa na Feliki kifungoni;

NDUGU, nia njema ya moyo wangu, na dua yangu niombayo Mungu kwa ajili ya Waisraeli ndio bii, waokolewe.

Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Na ingekuwa kheri kama mngalimiliki, illi sisi nasi tumiliki pamoja nanyi.

Maana nipendalo ni watu wote wawe kama mimi nilivyo; illakini killa mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.

INGEKUWA kheri kama mngenisamehe kidogo upumbavu wangu; naam, kanisameheni.

kwayo ni mjumbe kifungoni; nipate ujasiri katika kunena jinsi nipaswavyo kusema.

ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo