Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 26:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Alipokuwa akijitetea hivi, Festo akasema kwa sauti kuu, Paolo, una wazimu, kusoma kwako kwingi kumekugenza akili zako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Paulo alipofika hapa katika kujitetea kwake, Festo alisema kwa sauti kubwa, “Paulo! Una wazimu! Kusoma kwako kwingi kunakutia wazimu!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Paulo alipofika hapa katika kujitetea kwake, Festo alisema kwa sauti kubwa, “Paulo! Una wazimu! Kusoma kwako kwingi kunakutia wazimu!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Paulo alipofika hapa katika kujitetea kwake, Festo alisema kwa sauti kubwa, “Paulo! Una wazimu! Kusoma kwako kwingi kunakutia wazimu!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Paulo alipokuwa akifanya utetezi huu, Festo akasema kwa sauti kubwa, “Paulo, wewe umerukwa na akili! Kusoma kwingi kunakufanya uwe kichaa!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Paulo alipokuwa akifanya utetezi huu, Festo akasema kwa sauti kubwa, “Paulo, wewe umerukwa na akili! Kusoma kwingi kunakufanya uwe kichaa!”

Tazama sura Nakili




Matendo 26:24
19 Marejeleo ya Msalaba  

Jamaa zake walipopata khabari wakatoka kwenda kumkamata: maana walinena, Amerukwa na akili.


Wayahudi wakastaajabu, wakinena, Amepataje huyo kujua elimu, nae hajasoma?


Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo?


Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele.


Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo.


ENYI wanaume, ndugu zangu ua baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea nafsi yangu mbele yemi sasa.


Na Paolo alipokuwa akitoa hoja zake katika khabari ya haki na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akafanya khofu akajihu, Sasa enenda zako, nami nikipata wasaa nitakuita tena.


Na miaka miwili ilipotimia. Feliki akampokea Porkio Festo atawale badala yake. Na Feliki, akitaka kuwafanyia Wayahudi fadhili, akamwacha Paolo amefungwa.


Na marra nyingi katika masunagogi mengi naliwaadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaonea hasira kama nina wazimu, nikawaudhi hatta katika miji ya ugenini.


bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu,


Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi wenye akili katika Kristo; sisi dhaifu, lakini ninyi hodari; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima.


Maana ikiwa tumerukwa na akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu; au ikiwa tunazo akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu.


na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo