Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 26:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Bassi nikiisha kuupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hatta leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, wala sisemi neno illa yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Lakini Mungu alinisaidia; na hivyo mpaka siku ya leo nimesimama imara nikitoa ushuhuda kwa wote, wakubwa na wadogo. Ninayosema ni yale ambayo manabii na Mose walisema yatatukia;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Lakini Mungu alinisaidia; na hivyo mpaka siku ya leo nimesimama imara nikitoa ushuhuda kwa wote, wakubwa na wadogo. Ninayosema ni yale ambayo manabii na Mose walisema yatatukia;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Lakini Mungu alinisaidia; na hivyo mpaka siku ya leo nimesimama imara nikitoa ushuhuda kwa wote, wakubwa na wadogo. Ninayosema ni yale ambayo manabii na Mose walisema yatatukia;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Hadi leo nimepata msaada kutoka kwa Mungu, na hivyo nasimama hapa nikishuhudia kwa wakubwa na wadogo. Sisemi chochote zaidi ya yale ambayo manabii na Musa walisema yatatukia:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Hadi leo nimepata msaada kutoka kwa Mungu, na hivyo nasimama hapa nikishuhudia kwa wakubwa na wadogo. Sisemi chochote zaidi ya yale ambayo manabii na Musa walisema yatatukia:

Tazama sura Nakili




Matendo 26:22
42 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.


maana nina ndugu watano; awashuhudie, wasije nao mahali hapa pa adhabu.


Akaanza toka Musa na manabii, akawafasiria katika maandiko yote mambo yaliyomkhusu yeye.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, na ndivyo ilivyompasa Kristo kuteswa, na kufufuka siku ya tatu;


Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo.


Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na na manabii, Yesu, mwana wa Yusuf, mtu wa Nazareti


Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia:


Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; maana yeye aliandika khahari zangu.


Huyu manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake killa amwaminiye atapewa ondoleo la dhambi.


Hatta walipomaliza yote aliyoandikiwa, wakamshusha katika mti, wakamweka kaburini.


Illa neno hili naliungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.


nikikuokoa na watu wako, na watu wa mataifa, ambao nakutuma kwao;


Na sasa ninasimama hapa nihukumiwe kwa ajili ya tumaini la ahadi waliyopewa baba zetu na Mungu,


Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni.


Sasa, lakini, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sharia, inashuhudiwa na torati na manabii,


Kwa maana naliwapasha khabari ya mambo niliyoyapokea, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;


na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;


tena adha zangu na mateso yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Lustra; killa namna ya adha niliyoistahimili: nae Bwana akaniokoa katika yote.


Na mataifa walighadhabika, ghadhabu yako ikaja, na wakati wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, nao walichao jina lako, wadogo na wakubwa, na wa kuwaharibu hawo waiharibuo inchi.


Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.


Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo