Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 26:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Lakini inuka, usimame, maana nimekutokea kwa sababu hii, nikuweke nwe mtumishi na shahidi wa mambo haya uliyoyaona, na wa mambo ambayo kwayo nitajidhihirisha kwako;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo na yale ambayo bado nitakuonesha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo na yale ambayo bado nitakuonesha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Haidhuru, inuka sasa; simama wima. Nimekutokea ili nikuweke rasmi kuwa mtumishi wangu. Utawathibitishia watu wengine mambo uliyoyaona leo na yale ambayo bado nitakuonesha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Sasa inuka usimame kwa miguu yako. Nimekutokea ili nikuteue uwe mtumishi na shahidi wa mambo ambayo umeyaona, na yale nitakayokuonesha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Sasa inuka usimame kwa miguu yako. Nimekutokea ili nikuteue uwe mtumishi na shahidi wa mambo ambayo umeyaona, na yale nitakayokuonyesha.

Tazama sura Nakili




Matendo 26:16
34 Marejeleo ya Msalaba  

kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi, ua watumishi wa lile neno tokea mwanzo,


akapata sehemu ya khuduma hii.


atwae sehemu yake ya khuduma hii na utume huu, alioukosa Yuda aende zake mahali pake.


Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.


Na baada ya kuwasalimu, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyotenda katika mataifa kwa khuduma yake.


Nikasema, Nifanye nini, Bwana? Bwana akaniambia, Simama, uende hatta Dameski, na huko utaambiwa khabari za mambo vote yaliyoamriwa uyafanye.


Usiku ule Bwana akasimama karibu nae, akasema, Uwe na moyo mkuu, Paolo; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia khabari zangu Yerusalemi, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi.


Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambae wewe unaniudhi.


na sisi tutadumu katika kumwomba Mungu na kulikhudumia Neno lake.


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


illi niwe kuhani wa Yesu Kristo katika watu wa mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu.


KWA sababu hiyo, kwa kuwa tuna khuduma hii, kwa jinsi tulivyorehemiwa, hatulegei;


Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, nae alitupa khuduma ya upatauisho;


Maana sikuipokea kwa mwana Adamu wala sikufundishwa na mtu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo.


Nami nalikwenda kwa kufunuliwa, nikawaeleza injili ile niikhubirivyo katika mataifa, lakini kwa faraglia kwa hao walio wenye sifa, isiwe labda napiga mbio burre au nalipiga mbio burre.


ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri ile, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache,


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


ambalo nimekuwa mkhudumu wake, kwa uwakili wa Mungu, niliopewa kwa faida yenu, nilitimize neno la Mungu;


kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu;


tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,


Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu aliyenitia nguvu, kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akiniweka katika khuduma yake;


Ukiwakumhusha ndugu hayo, utakuwa mkhudumu mwema wa Yesu Kristo, na mzoevu wa maneno ya imani, na ya mafundisho yale mazuri uliyoyafuata.


Bali wewe erevuka katika yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mwinjilisti, timiliza khuduma yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo