Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 26:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Tukaanguka chini sote, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, Saul! Saul! ya nini kunindhi? ni vigumu kwako kunpiga mateke mchokoo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: ‘Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama ng'ombe anayepiga teke fimbo ya bwana wake.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: ‘Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama ng'ombe anayepiga teke fimbo ya bwana wake.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Sisi sote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikiniambia kwa Kiebrania: ‘Saulo, Saulo! Kwa nini unanitesa? Unajiumiza bure kama ng'ombe anayepiga teke fimbo ya bwana wake.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Wote tulianguka chini, nami nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, ‘Sauli, Sauli, mbona unanitesa? Ni vigumu kwako kuupiga teke mchokoo.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Wote tulipokuwa tumeanguka chini, nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya Kiebrania, ‘Sauli, Sauli, mbona unanitesa? Ni vigumu kwako kuupiga teke mchokoo.’

Tazama sura Nakili

Matendo 26:14
11 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, alipompa rukhusa, Paolo akasimama madarajani, akawapunjia mkono wale wenyeji; na ilipokuwa kimya kabisa, akanena nao kwa lugha ya Kiebrania, akisema,

Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza: akanena,

Ee Mfalme, wakati wa adhdhuhuri njiani naliona nuru inatoka mbinguni ipitayo mwangaza wa jua, ikinimulikia mimi, na wale waliofuatana nami pande zote.

Nami nikasema, Wewe u nani, Bwana? Bwana akaniambia, Mimi ni Yesu, ambae wewe unaniudhi.

Na watu waliosafiri pamoja nae wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu.

Au twamtia Bwana wivu? au tuna nguvu zaidi ya yeye?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo