Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 26:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Na marra nyingi katika masunagogi mengi naliwaadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaonea hasira kama nina wazimu, nikawaudhi hatta katika miji ya ugenini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mara nyingi niliwafanya waadhibiwe katika masunagogi yote nikiwashurutisha waikane imani yao. Hasira yangu kwao ilikuwa kubwa hata nikawasaka mpaka miji ya mbali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mara nyingi niliwafanya waadhibiwe katika masunagogi yote nikiwashurutisha waikane imani yao. Hasira yangu kwao ilikuwa kubwa hata nikawasaka mpaka miji ya mbali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mara nyingi niliwafanya waadhibiwe katika masunagogi yote nikiwashurutisha waikane imani yao. Hasira yangu kwao ilikuwa kubwa hata nikawasaka mpaka miji ya mbali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mara nyingi nilienda kutoka sinagogi moja hadi lingine nikiamuru waadhibiwe, nami nilijaribu kuwalazimisha wakufuru. Katika shauku yangu dhidi yao, hata nilienda miji ya kigeni ili kuwatesa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Mara nyingi nilikwenda kutoka sinagogi moja hadi ingine nikiamuru waadhibiwe, nami nilijaribu kuwalazimisha wakufuru. Katika shauku yangu dhidi yao, hata nilikwenda miji ya kigeni ili kuwatesa.

Tazama sura Nakili




Matendo 26:11
17 Marejeleo ya Msalaba  

Jihadharini na wana Adamu; kwa maana watawapelekeni mbele ya baraza, na katika masunagogi yao watawapiga;


Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.


Amin, nawaambieni, Dbambi zote watasamehewa wana Adamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;


Hatta alipojirudia nafsi yake, akasema, Watumishi wa mshahara wangapi wa baba yangu wanakula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.


Lakini kabla ya haya yote watawakamateni na kuwaudhini, watawapelekeni mbele ya sunagogi na gerezani, mkichukuliwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.


Akatenda hivyo. Mkono wake ukapona, ukawa mzima kama wa pili. Nao wakatekewa moyo: wakisemezana wao kwa wao, wamtendeje Yesu.


Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.


Walipopingamana nae na kutukana, akakungʼuta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu: mimi ni safi: langu sasa nitakwenda kwa watu wa mataifa.


Nami nikasema, Bwana, wanajua hao ya kuwa mimi nalikuwa nikwafunga wale wanaokuamini na kuwapiga katika masunagogi yao.


Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.


LAKINI Saul, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea kuhani mkuu,


Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa?


lakini alikaripiwa kwa ukhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo