Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 25:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 hali walikuwa na maswali juu yake katika dini yao wenyewe, na katika khabari ya mtu mmoja Yesu, aliyekuwa amekwisha kufa, ambae Paolo alishika kusema kwamba yu hayi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Ila tu walikuwa na mabishano kadhaa pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu mmoja aitwaye Yesu ambaye alikufa, lakini Paulo anashikilia kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Badala yake walikuwa na vipengele fulani vya kutokukubaliana naye kuhusu dini yao na kuhusu mtu aitwaye Isa aliyekufa, lakini Paulo alidai kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Badala yake walikuwa na vipengele fulani vya kutokukubaliana naye kuhusu dini yao na juu ya mtu mmoja aitwaye Isa, ambaye alikufa, lakini yeye Paulo alidai kwamba yu hai.

Tazama sura Nakili




Matendo 25:19
14 Marejeleo ya Msalaba  

akianza tangu ubatizo wa Yohana, hatta siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, lazima mmoja wao afanywe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.


Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


bali ikiwa ni hoja juu ya maneno na majina na sharia yenu, liangalieni ninyi wenyewe, maana mimi sitaki kuwa mwamuzi wa mambo hayo.


Wakalika Efeso, akawaacha huko. Yeye mwenyewe akaingia katika sunagogi, akahujiana na Wayahudi.


Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.


nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sharia yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa.


Na wale waliomshitaki waliposimama karibu nae, hawakumshitaki neno baya, kama nilivyodhani,


Walipokuja Wayahudi walioshuka kutoka Yerusalemi wakasimama karibu yake wakaleta mashitaka mengi na mazito juu yake, wasiyoweza kuyathuhutisha.


Khassa kwa sababu wewe unajua sana desturi na maswali yote waliyo nayo Wayahudi: kwa sababu hiyo nakuomba unisikilize kwa uvumilivu.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo