Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 25:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Bassi Festo alipokwisha kusema na watu wa baraza, akajibu, Umetaka rufaani kwa Kaisari! bassi, utakwenda kwa Kaisari.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Basi, baada ya Festo kuzungumza na washauri wake, akamwambia Paulo, “Umekata rufani kwa Kaisari, basi, utakwenda kwa Kaisari.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Basi, baada ya Festo kuzungumza na washauri wake, akamwambia Paulo, “Umekata rufani kwa Kaisari, basi, utakwenda kwa Kaisari.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Basi, baada ya Festo kuzungumza na washauri wake, akamwambia Paulo, “Umekata rufani kwa Kaisari, basi, utakwenda kwa Kaisari.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Baada ya Festo kufanya shauri pamoja na baraza lake, akatangaza, “Wewe umeomba rufaa kwa Kaisari, nako kwa Kaisari utaenda!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Baada ya Festo kufanya shauri pamoja na baraza lake, akatangaza, “Wewe umeomba rufaa kwa Kaisari, nako kwa Kaisari utakwenda!”

Tazama sura Nakili




Matendo 25:12
17 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, au si halali?


Mambo hayo yalipokwisha kumalizika, Paolo akaazimu rohoni mwake kupita kati ya Makedonia na Akaia aende Yerusalemi, akisema, Baada ya kuwako huko, yanipasa kuuona na Rumi.


Usiku ule Bwana akasimama karibu nae, akasema, Uwe na moyo mkuu, Paolo; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia khabari zangu Yerusalemi, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi.


Ikiwa nimekosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; hali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezae kunitia mikononi mwao. Nataka rufaani kwa Kaisari.


Siku kadha wa kadha zilipokwisha kupita, Agrippa mfalme na Bereniki wakafika Kaisaria, wakimwamkia Festo.


Lakini Paolo alipodai kuwekwa ahukumiwe na Augusto, nikaamuru alindwe hatta nitakapompeleka kwa Kaisari.


Agrippa akamwambia Festo, Mtu huyo angeweza kufunguliwa kama asingalitaka rufaani kwa Kaisari.


BASSI ilipoamriwa tusafiri hatta Italia, wakamtia Paolo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.


Tulipoingia Rumi akida akawatia wafungwa katika mikono ya jemadari wa walinzi wa Praitorio: bali Paolo alipewa rukhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda.


kama nilivyotazamia sana, na kutumaini, kwamba sitaaibika kabisa, bali kwa nthabiti wote, kama siku zote, na sasa tena Kristo atatukuzwa katika mwili wangu, ikiwa kwa maisha yangu, au kwa mauti yangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo