Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 25:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Ikiwa nimekosa au nimetenda neno la kustahili kufa, sikatai kufa; hali, kama si kweli neno hili wanalonishitaki, hapana awezae kunitia mikononi mwao. Nataka rufaani kwa Kaisari.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Basi, ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo, siombi kusamehewa adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watu hawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa Kaisari!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Basi, ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo, siombi kusamehewa adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watu hawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa Kaisari!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Basi, ikiwa nimepatikana na kosa linalostahili adhabu ya kifo, siombi kusamehewa adhabu hiyo. Lakini kama hakuna ukweli katika mashtaka waliyotoa watu hawa, hakuna awezaye kunikabidhi kwao. Nakata rufani kwa Kaisari!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Basi kama mimi nina hatia ya kutenda kosa lolote linalostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama mashtaka yaliyoletwa dhidi yangu na hawa Wayahudi si kweli, hakuna yeyote aliye na haki ya kunikabidhi mikononi mwao. Naomba rufaa kwa Kaisari!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

Matendo 25:11
17 Marejeleo ya Msalaba  

Paolo akawaambia, Wametupiga mbele ya watu wote bila kutuhukumu, na sisi tu Warumi, teua wametutupa gerezani; na sasa wanataka kututoa kwa siri? la, sivyo, na waje wenyewe wakatutoe.

Na Paolo alipotaka kufunua kinywa chake, Gallio akawaambia Wayahudi, Kama lingetendeka tendo la dhuluma au la hila mbaya, enyi Wayahudi, ingekuwa haki kuchukuliana nanyi;

Hatta walipokwisha kumfunga kwa kamba, Paolo akamwambia akida aliyesimama karibu, Je! ni halali kumpiga mtu Mrumi nae hajahukumiwa bado?

Paolo akasema, Mimi ninasimama hapa mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari, panipasapo kuhukumiwa: sikuwakosa Wayahudi neno, kama wewe ujuavyo sana.

Bassi Festo alipokwisha kusema na watu wa baraza, akajibu, Umetaka rufaani kwa Kaisari! bassi, utakwenda kwa Kaisari.

Lakini Paolo alipodai kuwekwa ahukumiwe na Augusto, nikaamuru alindwe hatta nitakapompeleka kwa Kaisari.

Nami nilipoona kama hakutenda neno la kustahili kuuawa, na yeye mwenyewe alipotaka kuhukumiwa na Augusto, nalikusudia kumpeleka kwake.

Agrippa akamwambia Festo, Mtu huyo angeweza kufunguliwa kama asingalitaka rufaani kwa Kaisari.

Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufaani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu.

waliomwua Bwana Yesu na manabii wao wenyewe na kutuudhi sisi, wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo