Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 24:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Na Paolo alipokuwa akitoa hoja zake katika khabari ya haki na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akafanya khofu akajihu, Sasa enenda zako, nami nikipata wasaa nitakuita tena.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Lakini wakati Paulo alipoanza kuongea juu ya uadilifu, juu ya kuwa na kiasi na juu ya siku ya hukumu inayokuja, Felisi aliogopa, akasema, “Kwa sasa unaweza kwenda; nitakuita tena nitakapopata nafasi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Lakini wakati Paulo alipoanza kuongea juu ya uadilifu, juu ya kuwa na kiasi na juu ya siku ya hukumu inayokuja, Felisi aliogopa, akasema, “Kwa sasa unaweza kwenda; nitakuita tena nitakapopata nafasi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Lakini wakati Paulo alipoanza kuongea juu ya uadilifu, juu ya kuwa na kiasi na juu ya siku ya hukumu inayokuja, Felisi aliogopa, akasema, “Kwa sasa unaweza kwenda; nitakuita tena nitakapopata nafasi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Naye Paulo alipokuwa akinena kuhusu haki, kuwa na kiasi na kuhusu hukumu ijayo, Feliksi aliingiwa na hofu, akasema, “Hiyo yatosha sasa! Unaweza kuondoka. Nitakapokuwa na muda, nitakuita.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Naye Paulo alipokuwa akinena juu ya haki, kuwa na kiasi na juu ya hukumu ijayo, Feliksi aliingiwa na hofu na kusema, “Hiyo yatosha sasa! Waweza kuondoka. Nitakapokuwa na wasaa nitakuita.”

Tazama sura Nakili




Matendo 24:25
99 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake:


Na akiisha kuja yeye, atauhakikisha ulimwengu kwa khabari ya dhambi, na haki, na hukumu;


Akatuagiza tuwakhubiri watu na kushuhudu ya kuwa huyu udiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa hayi na wafu.


Lakini Wayahudi wa Thessaloniki walipopata khabari ya kwamba Neno la Mungu linakhubiriwa na Paolo katika Beroya, wakaenda huko wakawachafua makutano.


Na Paolo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahujiana nao kwa maneno yii maandiko sabato tatu,


Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo.


Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?


Nina tumaini kwa Mungu, na hatta hao nao wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa ufufuo wa wafu wenye haki na wasio haki pia.


Tena alitaraja kwamba atapewa fedha na Paolo illi amfungue: kwa hiyo alimwita marra nyingi akaongea nae.


Agrippa akamwambia Paolo, Kwa maneno machache wataka kunifanya kuwa Mkristo.


Lakini simama, uingie mjini, utaambiwa yatakayokupasa kutenda.


BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana.


Bassi kama ni hivyo, killa mtu miongoni mwetu atatoa khabari za nafsi yake mbele za Mungu.


katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wana Adamu, sawa sawa na injili yangu, kwa Yesu Kristo.


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya.


(maana anena, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokofu nilikusaidia; tazama, sasa ndio wakati uliokubalika sana; tazama, sasa ndio siku ya wokofu).


Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi waaminio wapewe ahadi kwa imani ya Yesu Kristo.


upole, kiasi; juu ya mambo ya jinsi hii hapana sharia.


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


bali awe mkaribishaji, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kujimudu nafsi yake;


Na baya yaliyoonekana yalikuwa ya kutisha, hatta Musa akasema, Nashikwa na khofu na kutetemeka.


Lakini muonyane killa siku, maadam iitwapo leo; mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.


BASSI, ikiwa ikaliko abadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.


na mafundisbo ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.


Na jinsi watu wanavyowekewa kufa marra moja, na baada ya kufa hukumu:


Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vyema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.


bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu; mwe tayari siku zote kumjibu killa mtu akuulizae khabari za tumaini lililo ndani yenu; kwa upole na kwa khofu,


na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu uvumilivu, na katika uvumilivu wenu utawa,


Hivi watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Shetani. Mtu aliye yote asiyefanya haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.


Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyae haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo