Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 24:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Bassi Feliki, alijiokwisha kusikia haya, aliwaakhirisha, kwa sababu alijua khabari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lusia jemadari, atakapotelemka nitakata maneno yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo njia vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, “Nitatoa hukumu juu ya kesi hiyo wakati Lusia, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo njia vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, “Nitatoa hukumu juu ya kesi hiyo wakati Lusia, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Hapo, Felisi, ambaye mwenyewe alikuwa anaifahamu hiyo njia vizuri, aliahirisha kesi hiyo. Akawaambia, “Nitatoa hukumu juu ya kesi hiyo wakati Lusia, mkuu wa jeshi, atakapokuja hapa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Basi Feliksi, ambaye alifahamu vizuri habari za Njia Ile, akaahirisha kesi ile, akasema, “Jemadari Lisia atakapoteremka huku, nitaamua kesi yenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Basi Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia ile, akaahirisha shauri lile kwa maelezo yake akisema, “Wakati jemadari Lisia atakapoteremka huku, nitaamua shauri lako.”

Tazama sura Nakili




Matendo 24:22
11 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Herode akawaita majusi kwa faragha, akapata kwao hakika ya muda ile nyota ilipoonekana.


Walipotaka akae wakati mwingi zaidi, hakukubali:


Kwa maana tuna khatari ya kushtakiwa fitina kwa ajili ya mambo haya ya leo, ikiwa hakuna sababu ambayo kwa ajili yake tutaweza kujiudhuru kwa mkutano huu.


Na liwali alipompungia mkono illi anene, Paolo akajibu, Kwa kuwa ninajua kama wewe umekuwa mwamuzi wa taifa hili kwa muda wa miaka mingi, najitetea nafsi yangu kwa moyo wa furaha.


Illa neno hili naliungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.


Baada ya siku kadha wa kadha, Feliki akafika pamoja na Drusilla mkewe aliyekuwa Myahudi, akamwita Paolo akamsikiliza khabari za imani ya Kristo.


Na tena alijaribu kuitia hekalu najis: tukamkamata: tukataka kumhukumu kwa sharia yetu.


Nami sina neno la hakika la kumwandikia Bwana. Kwa hiyo nimemleta hapa mbele yenu, illi akiisha kuulizwa khabari zake, nipate neno la kuandika.


Khassa kwa sababu wewe unajua sana desturi na maswali yote waliyo nayo Wayahudi: kwa sababu hiyo nakuomba unisikilize kwa uvumilivu.


akataka ampe khati za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masunagogi, illi akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo