Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 23:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Pakawa makelele mengi. Waandishi wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakamtetea, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema nae tusishindane na Mungu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kelele ziliongezeka na baadhi ya waalimu wa sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kelele ziliongezeka na baadhi ya waalimu wa sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kelele ziliongezeka na baadhi ya waalimu wa sheria wa kikundi cha Mafarisayo walisimama na kutoa malalamiko yao kwa nguvu: “Hatuoni chochote kilicho kiovu katika mtu huyu; huenda ikawa kwamba roho au malaika ameongea naye.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Kukawa na ghasia kubwa, nao baadhi ya walimu wa Torati ambao ni Mafarisayo, wakasimama wakapinga kwa nguvu wakisema, “Hatuoni kosa lolote la mtu huyu! Huenda ikawa roho au malaika amezungumza naye”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Kukawa na ghasia kubwa, nao baadhi ya walimu wa Torati ambao ni Mafarisayo, wakasimama wakapinga kwa nguvu wakisema, “Hatuoni kosa lolote la mtu huyu! Huenda ikawa roho au malaika amezungumza naye”

Tazama sura Nakili

Matendo 23:9
23 Marejeleo ya Msalaba  

Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Kwa nini anakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

Nae akawaambia marra ya tatu, Kwani? ubaya gani alioutenda huyu? sikuona hatta neno kwake la kustahili kufa; bassi nikiisha kumrudi nitamfungua.

Pilato akawaambia makuhani wakuu na makutano, Mimi sioni khatiya yo yote katika mtu huyu.

Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

Bassi makutano waliosimama karibu wakasikia, wakanena kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema nae.

Bassi ikiwa Mwenyiezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?

Ikawa nilipokuwa nikisafiri, nikikaribia Dameski, wakati wa adhdhuhuri, ghafula nuru kuu ilitoka mbinguni, ikanimulikia pande zote.

Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, Saul, Saul, Mbona unaniudhi?

nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sharia yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa.

Kwa maana Masadukayo husema ya kwamba hakuna kiyama wala malaika na roho: bali Mafarisayo hukiri yote mawili.

Nami nilipoona kama hakutenda neno la kustahili kuuawa, na yeye mwenyewe alipotaka kuhukumiwa na Augusto, nalikusudia kumpeleka kwake.

wakaenda mbali kidogo wakasemezana, wakisema, ya kama, Mtu huyo hatendi neno linalostahili kifo wala kufungwa.

Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambae mimi ni mtu wake, na udiye nimtumikiae, alisimama karibu nami akaniambia,

illakini ikiwa ya Mungu hamwezi kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu.

Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Saul, Saul, mbona wanifukuza?

Au twamtia Bwana wivu? au tuna nguvu zaidi ya yeye?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo