Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 23:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Paolo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Mafarisayo, na sehemu ya pili Masadukayo, akapaaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana wa Farisayo: mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Wakati huo Paulo alikwisha tambua kwamba sehemu moja ya wanabaraza wale ilikuwa ni Masadukayo na nyingine Mafarisayo. Basi, alipaza sauti yake mbele ya Baraza, “Ndugu zangu, mimi ni Mfarisayo, mwana wa Mfarisayo. Mimi nimeletwa mahakamani kwa kuwa ninatumaini kwamba wafu watafufuka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Wakati huo Paulo alikwisha tambua kwamba sehemu moja ya wanabaraza wale ilikuwa ni Masadukayo na nyingine Mafarisayo. Basi, alipaza sauti yake mbele ya Baraza, “Ndugu zangu, mimi ni Mfarisayo, mwana wa Mfarisayo. Mimi nimeletwa mahakamani kwa kuwa ninatumaini kwamba wafu watafufuka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Wakati huo Paulo alikwisha tambua kwamba sehemu moja ya wanabaraza wale ilikuwa ni Masadukayo na nyingine Mafarisayo. Basi, alipaza sauti yake mbele ya Baraza, “Ndugu zangu, mimi ni Mfarisayo, mwana wa Mfarisayo. Mimi nimeletwa mahakamani kwa kuwa ninatumaini kwamba wafu watafufuka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Paulo alipotambua ya kuwa baadhi yao walikuwa Masadukayo na wengine ni Mafarisayo, akapaza sauti kwenye Baraza la Wayahudi, akasema, “Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana Farisayo. Hapa nimeshtakiwa kuhusu tumaini langu katika ufufuo wa wafu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Paulo alipotambua ya kuwa baadhi yao walikuwa Masadukayo na wengine ni Mafarisayo, akapaza sauti kwenye baraza, “Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana Farisayo. Hapa nimeshtakiwa kuhusu tumaini langu katika ufufuo wa wafu.”

Tazama sura Nakili




Matendo 23:6
17 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni, mimi nawatumeni kama kondoo kati ya mbwa wa mwitu: bassi mwe na busara kama nyoka, na msio na dhara kama hua.


Siku ile Masadukayo, watu wanenao kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,


Hatta akiona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, akawaambia, Uzao wa nyoka, nani aliyewaonya mkimbie ghadhabu ijayo?


Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, nikalelewa katika niji huu miguumi pa Gamaliel, nikafundishwa sharia ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa ijtihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi:


Siku ya pili yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru makuhani wakuu na baraza yote waje. Akamleta Paolo chini, akamweka mbele yao.


Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.


PAOLO akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa nia safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hatta leo hivi.


Bassi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua khabari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia.


Akasema, Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paolo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata khabari zake kwa usahihi zaidi. Bassi wewe usikubali;


Alipokwisha kunena hayo palikuwa na fitina beina ya Mafarisayo na Masadukayo, mkutano ukagawanyika.


Nina tumaini kwa Mungu, na hatta hao nao wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa ufufuo wa wafu wenye haki na wasio haki pia.


isipokuwa kwa ajili ya sauti hii moja, nilipolia nikisimama katikati yao, Kwa ajili ya ufufuo wa wafu ninahukumiwa mbele yenu hivi leo.


Bassi kwa ajili ya hayo, nimewaiteni mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli.


Nalitabiriwa siku ya nane, ni lutu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benjamin, Mwebrania wa Waebrania, kwa khabari ya kuifuata sharia, Farisayo, kwa khabari ya wivu, mwenye kuliudhi Kanisa,


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo mle mlimo ndani ya pazia,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo