Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 23:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Hatta nilipopewa khabari kwamba patakuwa na vitimbi juu ya mtu huyu, marra nikampeleka kwako, nikawaagiza na wale walioshitaki, wanene khabari zake mbele yako. Salamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za kumwua, niliamua kumleta kwako, nikawaambia washtaki wake walete mashtaka yao mbele yako.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za kumwua, niliamua kumleta kwako, nikawaambia washtaki wake walete mashtaka yao mbele yako.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Nilipofahamishwa kwamba Wayahudi walikuwa wamefanya njama za kumwua, niliamua kumleta kwako, nikawaambia washtaki wake walete mashtaka yao mbele yako.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Nilipoarifiwa kuwa kulikuwa na njama dhidi ya mtu huyu, nilimtuma kwako mara moja. Niliwaagiza washtaki wake pia waeleze mashtaka yao dhidi yake mbele yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Nilipoarifiwa kuwa kulikuwa na shauri baya dhidi ya mtu huyu, nilimtuma kwako mara moja. Niliwaagiza washtaki wake pia waeleze mashtaka yao dhidi yake mbele yako.

Tazama sura Nakili




Matendo 23:30
11 Marejeleo ya Msalaba  

mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongwa, na asharati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Salamu.


Kulipopambazuka, baadhi ya Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo wakisema. Hatuli wala hatunywi hatta tutakapokwisha kumwua Paolo.


Akasema, Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paolo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata khabari zake kwa usahihi zaidi. Bassi wewe usikubali;


Bassi, wale askari wakamchukua Paolo kamu walivyoamriwa, wakampeleka hatta Antipatri usiku:


Nitakusikia maneno yako watakapokuja wale waliokushitaki; akaamuru alindwe katika praitorio ya Herode.


Imewapasa hao kuwapo hapa mbele yako na kunishitaki kama wana neno lo lote juu yangu.


Nikawajibu kwamba sio desturi ya Warumi kumtoa mtu aliye yote auawe, kabla mtu yule aliyeshitakiwa hajaonana na washitaki wake uso kwa uso, na kupewa nafasi ya kujitetea katika mashitaka yake.


lakini hila yao ikajulikana na Saul. Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua.


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo