Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 23:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Mjomba wake Paolo akasikia khabari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paolo khabari.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Lakini mtoto wa ndugu yake Paulo alisikia juu ya mpango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Lakini mtoto wa ndugu yake Paulo alisikia juu ya mpango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Lakini mtoto wa ndugu yake Paulo alisikia juu ya mpango huo; hivyo akaenda ndani ya ngome, akamjulisha Paulo juu ya njama hiyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Lakini mtoto wa dada yake Paulo aliposikia kuhusu njama hiyo, alienda kule kwenye ngome ya askari na kumweleza Paulo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Lakini mtoto wa dada yake Paulo aliposikia juu ya shauri hilo baya, alikwenda kule kwenye ngome ya askari na kumweleza Paulo.

Tazama sura Nakili




Matendo 23:16
12 Marejeleo ya Msalaba  

Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Bassi alipokuwa hawezi kupata hakika ya khabari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.


Na Paolo alipokuwa anaingizwa ndani ya ngome, akamwambia jemadari, Nina rukhusa nikuambie neno? Nae akasema, Je! unajua Kiyunani?


Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paolo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumpokonya mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.


Paolo akamwita akida mmoja, akasema, Mchukue huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwarifu.


hatta assubuhi wakawaacha wale wapanda farasi waende pamoja nae, nao wakarudi zao ngomeni.


Akamwamuru yule akida amlinde Paolo; illa awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumkhudumu au kuja kumtazama.


Maana hekima ya dunia hii ni upumbavu mbele ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, Yeye ndiye awanasae wenye hekima katika hila yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo