Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 23:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PAOLO akawakazia macho watu wa baraza, akasema, Ndugu zangu, mimi kwa nia safi kabisa nimeishi mbele za Mungu hatta leo hivi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Paulo aliwakodolea macho wale wanabaraza, halafu akaanza kusema, “Ndugu zangu, mpaka hivi leo nimekuwa nikiishi na dhamiri njema mbele ya Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Paulo aliwakodolea macho wale wanabaraza, halafu akaanza kusema, “Ndugu zangu, mpaka hivi leo nimekuwa nikiishi na dhamiri njema mbele ya Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Paulo aliwakodolea macho wale wanabaraza, halafu akaanza kusema, “Ndugu zangu, mpaka hivi leo nimekuwa nikiishi na dhamiri njema mbele ya Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Paulo akawakazia macho wale wajumbe wa Baraza la Wayahudi, akasema, “Ndugu zangu, nimetimiza wajibu wangu kwa Mungu kwa dhamiri safi kabisa hadi leo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Paulo akawakazia macho wale wajumbe wa baraza, akasema, “Ndugu zangu, nimetimiza wajibu wangu kwa Mungu kwa dhamiri safi kabisa hadi leo.”

Tazama sura Nakili




Matendo 23:1
17 Marejeleo ya Msalaba  

Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto.


ENYI wanaume, ndugu zangu ua baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea nafsi yangu mbele yemi sasa.


Siku ya pili yake akitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru makuhani wakuu na baraza yote waje. Akamleta Paolo chini, akamweka mbele yao.


Kama kuhani mkuu nae anishuhudiavyo, na wazee wa baraza wote pia, ambao nalipewa barua nao kwa ndugu zao, nikaenda Dameski, illi niwalete wale waliokuwa huko hatta Yerusalemi, wamefungwa waadhibiwe.


Bassi sasa ninyi pamoja na wazee wa baraza mwambieni jemadari amlete chini kwenu, kana kwamba mnataka kujua khabari zake vizuri zaidi; na sisi tu tayari kumwua kabla hajakaribia.


Akasema, Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paolo chini kesho, ukamweke mbele ya baraza, kana kwamba wanataka kupata khabari zake kwa usahihi zaidi. Bassi wewe usikubali;


Na nikitaka kuijua sababu hatta wakamshitaki, nikamleta chini nikamweka mbele ya baraza:


Paolo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Mafarisayo, na sehemu ya pili Masadukayo, akapaaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana wa Farisayo: mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu.


Nami ninajizoeza katika neno hili kuwa na dhamiri isiyo na khatiya mbele ya Mungu na mbele ya watu.


Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika.


Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabikiwi haki kwa ajili hiyo; illa aninukumuye ni Bwana.


Hwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri yetu, ya kwamba kwa unyofu na weupe wa moyo utokao kwa Mungu, si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya Mungu, tulienenda katika dunia, na khassa kwenu ninyi.


lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyosetirika, wala hatuenendi kwa ujanja, wala kulichanganya neno la Mungu na uwongo; hali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mhele za Mungu.


Namshukuru Mungu, nimwabuduye tangu zamani za wazee wangu kwa dhamiri safi, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu, mchana na usiku, ninatamani sana kukuona,


Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote.


mkiwa na dhamiri njema, illi katika neno lile mnalosingiziwa kwamba m watenda mabaya, wataha yarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo